Home news HILO HAPA BENCHI LA SIMBA MSIMU WA 2021/22

HILO HAPA BENCHI LA SIMBA MSIMU WA 2021/22


MSIMU wa 2021/22 unatarajiwa kuanza Septemba 27 ambapo tayari ratiba ipo wazi baada ya Bodi ya Ligi Tanzania,  (TPLB) kuweza kuiweka wazi.

Septemba 25 ni mchezo wa Ngao ya Jamii ambapo Simba itamenyana na Yanga, Uwanja wa Mkapa.

Hili hapa ni bechi la ufundi la Klabu ya Simba  msimu wa 2021/22 ambalo litakuwa na kazi ya kutetea taji ya Ngao ya Jamii mbele ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi:-

Didier Gomes huyu ni Kocha Mkuu wa Simba.

Thiery Hitimana huyu ni Kocha Msaidizi akiwa sambamba na Seleman Matola.

Aishi Manula, Beno Kakolanya, Jeremiah Kisubi hawa makipa watanolewa na Milton Nienov.

Adel Zrane huyu mwamba ni Kocha wa Viungo.

Calvin Mavhunga, huyu ni Mtalaamu wa Tathmini za mechi zote za Simba ambapo anawafuatilia wapinzani na wachezaji wa Simba pia.

Dr Yassin Gembe huyu ni Dokta wa timu,

Fareed Cassem huyu ni mtalamu wa misuli

Abass Ally mratibu wa timu. 

Patrick Rweyemamu ni Meneja.

Hamis Mtambo Kit Meneja  sawa na Jallow Bakari . 

SOMA NA HII  JAMBO LA PHIRI BADO NDANI YA SIMBA....KAULI YA KLABU IMESIMAMIA UPANDE HUU...