Home news HUYU HAPA MUNGU KAMPA NEEMA YA UMRI MREFU ATAKIWASHA SIMBA V YANGA

HUYU HAPA MUNGU KAMPA NEEMA YA UMRI MREFU ATAKIWASHA SIMBA V YANGA


 KWENYE mchezo wa leo wa Ngao ya Jamii kati ya Simba v Yanga  ni nyota mmoja ambaye amewakimbiza wote kwa kuwa na mwili jumba pamoja na Mungu kumpa neema ya kucheza akiwa na umri mkubwa.

Ni Pascal Wawa nyota wa Simba rekodi zinaonyesha kwamba amewakimbiza wengi kwa kuishi muda mrefu duniani na bado anacheza kama kawaida bila mashaka.

Aliletwa duniani mwaka 1986 ilikuwa ni Januari Mosi hivyo umri wake unasoma miaka 35. 

Ni jambo la msingi kuwa na wachezaji wenye umri ambao wanacheza kwa kuwa wanatoa somo kwamba kila kitu kinawezekana na jambo la msingi kwa wachezaji ni lazima kutunza afya zao pamoja na kufanya mazoezi bila kuchoka.

Wawa ni beki wa kati tegemeo ndani ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes na huenda leo akaanza kikosi cha kwanza kama kawaida.

Mwamba huyu ni raia wa Ivory Coast huwa haishiwi mbwembwe awapo uwanjani na ni namba moja kwa kupiga mipira mirefu yenye macho akiwa ndani ya uwanja.

Saa 11:00 Uwanja wa Mkapa ni Simba v Yanga, Ngao ya Jamii.

SOMA NA HII  KAMA UNA HALOTEL HII INAKUHUSU....MERIDIANBET WATAKUPA 'MSHIKO' KILA SIKU....