Home news IMEFICHUKA…KIGOGO SIMBA AFUNGUKA TIMU ITAKAYOCHEZA NA SIMBA KWENYE SIMBA DAY..ATAJA ‘SAPRAIZI’

IMEFICHUKA…KIGOGO SIMBA AFUNGUKA TIMU ITAKAYOCHEZA NA SIMBA KWENYE SIMBA DAY..ATAJA ‘SAPRAIZI’


Kaimu Afisa Habari wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Ezekiel Kamwaga amewaomba Mashabiki na Wanachama wa Klabu hiyo kujiandaa vizuri, kuelekea Tamasjha ya Simba Day.

Tayari Uongozi wa Simba SC umetangaza Septemba 19 kuwa siku maalum ya Tamasha hilo mwaka mwaka huu 2021, huku taarifa zikieleza kuwa Uongozi wa Mabingwa hao umepanga kufanya kitu kikubwa.

Kamwaga amesema dhamira kubwa ya Simba SC kwa mwaka huu 2021 ni kufanya kitu cha tofauti katika Tamasha la Simba Day, hivyo Mashabiki na Wanachama wanapaswa kuwa tayari kwa siku hiyo.

Amesema mpaka sasa wameshapokea maombi ya klabu kadhaa ambazo zinapenda kushiriki katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya kikosi cha Simba SC, ambao utakuwa sehemu za Shamra Shamra za siku hiyo.

“Simba Day ya mwaka huu itakuwa kubwa. Mpaka sasa tumeshapokea maombi ya timu ambazo zimeshashinda ubingwa wa Afrika zaidi ya mara mbili. Nawahakikishia Simba itacheza na timu kubwa sana barani Afrika katika Simba Day 2021”

Uongozi wa Simba SC hulitumia Tamasha la Simba Day, kutambulisha wachezaji wapya waliosajiliwa kwa msimu unaofuata, burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali na kucheza mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki.

SOMA NA HII  SIKU CHACHE BAADA YA KUSAMEHEWA...MORISSON ALIZUA TENA SIMBA...AMVIMBIA MENEJA WA TIMU...