Home Azam FC KOCHA AZAM FC AKUBALI KUWA MUUNGANIKO BADO TATIZO

KOCHA AZAM FC AKUBALI KUWA MUUNGANIKO BADO TATIZO




 BENCHI la ufundi la Azam FC limeweka wazi kwamba bado hakujawa na maelewano mazuri kati ya kiungo Idd Seleman, ‘Nado’ na mshambuliaji mpya Idris Mbombo jambo ambalo watalifanyia kazi kwa umakini.


Juzi, Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Horseed FC ya Somalia kwenye mchezo wa awali wa Kombe la Shirikisho uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Ni mabao ya Ayub Lyanga kwa kichwa dakika ya 32 aliyefunga kwa kutumia pasi ya Nado,Mbombo dakika ya 72 aliyefunga kwa pasi ya Salum Abubakar, ‘Sure Boy’ aliyekuwa nahodha kwenye mchezo huo na lile la tatu lilipachikwa na Lusajo Mwaikenda dakika ya 78 na lile la Horseed lilipachikwa na IbrahimNor dk 22.

Kocha Msaidizi wa Azam FC, Vivier Bahati amesema kuwa Nado alikuwa akifanya kazi kubwa ya kutengeneza nafasi ila zilikuwa zinashindwa kufika sehemu sahihi mara kwa mara.

“Kuhusu Nado alikuwa anatengeneza nafasi nyingi ila zimeshindwa kubadilishwa kuwa mabao na hii inatokana na kutokuwa na maelewano yakutosha kati yake na Mbombo, tofauti na ilivyokuwa kwa Prince Dube.

“Kwa muda unavyozidi kwenda imani yetu ni kuona kwamba wanakuwa kitu kimoja na tunaamini kwamba watafanya vizuri kwani wote ni wachezaji wa timu moja na wana uwezo mkubwa hivyo ni suala la kusubiri,” amesema Vivier.

Azam FC wanatarajiwa kumenyana na timu hiyo kwa mara nyingine ikiwa ni mchezo wa marudio, Septemba 18, Uwanja wa Azam Complex.

SOMA NA HII  SIKU CHACHE TOKA AJIUNGE NA AZAM...SOPU AFUNGUKA A-Z JINSI ALIVYOZIPIGA CHENGA OFA ZA SIMBA NA YANGA...