Home CAF KUELEKEA MICHUANO YA KLABU BINGWA AFRIKA NA SHIRIKISHO..CAF WASHUSHA RUNGU TZ..WAFUNGIA UWANJA

KUELEKEA MICHUANO YA KLABU BINGWA AFRIKA NA SHIRIKISHO..CAF WASHUSHA RUNGU TZ..WAFUNGIA UWANJA

[the_ad id="25893"]


Shirikisho la soka Barani Afrika CAF limeupiga chini Uwanja wa CCM Kirumba kutumika kwa ajili ya michuano ya Kimataifa msimu wa 2021/22.

Uwanja wa CCM Kirumba ulitarajiwa kutumiwa na timu ya Biashara United Mara kwa ajili ya michezo ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika itakayoanza baadae mwezi huu.

Meneja na mratibu wa Biashara United Mara amesema wamepokea taarifa za kukataliwa kwa Uwanja huo, hivyo wamelazimika kubadili kila kitu, kwani walikuwa Kirumba kwa zaidi ya siku 10 na wachezaji walikuwa wamezoea mazingira.

Biashara United Mara itaanzia nyumbani kwa kucheza dhidi ya FC Dikhil ya Djibouti, na ni rasmi sasa mpambano huo utapigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here