Home news KUMBE MUUAJI WA SIMBA ALIPANIA KUFANYA HIVYO

KUMBE MUUAJI WA SIMBA ALIPANIA KUFANYA HIVYO


 MSHAMBULIAJI wa Yanga, Fiston Mayele amesema kuwa ilikuwa ni malengo yake tangu mwanzo kufunga bao mbele ya Simba ili aweze kuongeza hali ya kujiamini.

Ikiwa ni mchezo wake wa kwanza kucheza akiwa na jezi ya Yanga, Uwaja wa Mkapa Mayele alipachika bao pekee la ushindi kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii kwa shuti kali ambalo lilimshinda kipa wa Simba Aishi Manula.

Kwa wakati huu mabingwa wa Ngao ya Jamii ni Yanga na wamewavua mabingwa watetezi wa Ngao ya Jamii, Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes.

Mayele amesema:”Ilikuwa kazi ngumu kwa kila mchezaji kupambana ili kupata matokeo lakini nilikuwa nahitaji kufunga ili kuongeza hali ya kujiamini.

“Kwa namna ambavyo ilikuwa kwangu mimi nilikuwa ninaomba nifunge kwa muda na imekuwa hivyo ni furaha kwangu na wachezaji kiujumla,”.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA JUMAPILI...RALLY BWALYA AFUNGUKA HAYA DHIDI YA WAZAMBIA WENZAKE