Home news KUELEKEA MECHI YA JUMAPILI…RALLY BWALYA AFUNGUKA HAYA DHIDI YA WAZAMBIA WENZAKE

KUELEKEA MECHI YA JUMAPILI…RALLY BWALYA AFUNGUKA HAYA DHIDI YA WAZAMBIA WENZAKE

 


Kiungo Mshambuliaji wa Simba SC Rally Bwalya amefunguka kuhusu wapinzani wao katika michuano ya Kombe la Shirikisho Red Arrows ambao wanatarajiwa kuwasili jijini Dar es salaam leo Ijumaa (Novemba 26).

Bwalya amesema anaifahamu vyema Red Arrows, na anatarajia mchezo mzuri kutoka kwenye timu hiyo ambayo aliwahi kucheza dhidi yake alipokua nchini Zambia.

Kiungo huyo kutoka nchini Zambia amesema Red Arrows sio timu mbaya, ina kikosi kizuri na ndio maana inashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, hivyo ni wajibu wao kama wachezaji wa Simba SC kujipanga vizuri na kucheza kwa tahadhari kubwa.

“Red Arrows si timu mbaya ndiyo maana imefika hatua hii na hatutaidharau, tutaingia uwanjani kupambana kutafuta ushindi tukijua tupo nyumbani. Tutaingia uwanjani kuhakikisha tunapambana kutafuta ushindi.

“Tulikuwa na nafasi ya kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa lakini ikashindikana, sasa tumepata tena nafasi ya kufanya hivyo kwenye Kombe la Shirikisho Afrika tutahakikisha inawezekana,” amesema Bwalya

Simba SC iliangukia kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, baada ya kutolewa kwenye Michuano ya Klabu Bingwa Afrika kwa kufungwa nyumbani Dar es salaam mabao 3-1 dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana.

Kabla ya mchezo huo Simba SC ilishinda ugenini mjini Gaborone mabao 2-0, hivyo Mabingwa hao wa Tanzania Bara walitupwa nje kwa kufungwa mabao mengi nyumbani.

SOMA NA HII  RAIS SAMIA AMWAGA NEEMA KWENYE MICHEZO..SIMBU ATAJWA