Home news NABI ATAKA ‘PIRA BIRIANI’ LA SIMBA NDANI YA YANGA…MCHEZAJI ATAKAYEZINGUA KUPIGWA BENCHI...

NABI ATAKA ‘PIRA BIRIANI’ LA SIMBA NDANI YA YANGA…MCHEZAJI ATAKAYEZINGUA KUPIGWA BENCHI MAZIMA….

 


KOCHA Mkuu wa Yanga Mtunisia, Nasreddine Nabi anataka kuona timu yake ikiendelea kucheza soka safi la kisasa la pasi nyingi kama jinsi ilivyokuwa ikicheza Simba misimu ya hivi karibuni na mchezaji akibutua mpira, basi benchi litamuhusu.

Hiyo ni baada ya kuanza vema katika msimu huu kwa kucheza soka la pasi nyingi wakati timu yake ikiwa na mpira ikishambulia goli la wapinzani.Yanga hivi sasa inaoongoza katika msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 15 ikicheza michezo mitano bila ya kupoteza wowote.

Akizungumza na gazeti la  Championi Jumatatu, Nabi alisema kuwa katika timu yake anataka awe na wachezaji wenye uwezo mkubwa wa umiliki wa mpira kama Yannick Bangala, Khalid Aucho na Feisal Salum ‘Fei Toto’.Nabi alisema kuwa ushindi pekee hautoshi katika timu yake, kikubwa anataka kuona timu inapata ushindi na soka safi la kuvutia pasi nyingi na siyo kubutua.

Aliongeza kuwa katika timu yake kama akiona aina ya wachezaji hao wanaobutua, ikitokea akatokea, basi benchi litamhusu katika kikosi chake.

“Napenda kuona wachezaji wangu wakiwapa burudani ya soka safi la kuvutia mashabiki wetu ambao kila siku wamekuwa wakijitokeza uwanjani kutusapoti.

“Hivyo burudani nzuri wanaipata kutokana na soka safi la pasi litakalofuatana na ushindi kwa ajili ya kujiongezea idadi ya pointi.

“Sitakuwa tayari kumtumia mchezaji ambaye hafuati kile ambacho kocha anakitaka, ni lazima acheze kwa kufuata maelekezo yangu ya soka la pasi na siyo kubutua,”alisema Nabi.

SOMA NA HII  WAPINZANI WAIPIGIA SALUTI YANGA...WAFUNGUKA HAYA