Home news LITOMBO ABADILISHIWA MAJUKUMU YANGA

LITOMBO ABADILISHIWA MAJUKUMU YANGA


 MKUU wa benchi la ufundi la Yanga, Nasreddine Nabi amesema kuwa licha ya mchezaji wake Yannick Bangala Litombo kucheza katika eneo la kiungo katika mchezo dhidi ya Zanaco lakini 
atamtumia zaidi katika eneo la beki wa kati.


Litombo katika mchezo wake 
wa kwanza kuitumikia Yanga alicheza katika eneo la kiungo mkabaji akichukua nafasi ya Mukoko Tonombe kipindi cha pili katika mchezo ambao Yanga walipoteza kwa idadi ya mabao 2-1 dhidi ya Zanaco.


Kwa maana hiyo Litombo atakuwa amebadilishiwa majukumu kwenye eneo la kucheza tofauti na nafasi ambayo alianza nayo ndani ya Yanga. 

Akizungumza na ChampionIjumaa, Nabi aliweka wazi kuwa licha ya uwezo mzuri aliouonyesha Litombo katika eneo la ukabaji lakini bado anayo nafasi kubwa ya kutumika katika eneo la beki wa kati kutokana na mahitaji ya timu kumhitaji mchezaji huyo katika eneo hilo.

 

“Kuhusu wapi nitamtumia Bangala Litombo ndani ya Yanga nadhani itatokana na mahitaji ya timu, amecheza vizuri katika eneo la kiungo lakini mahitaji makubwa ya timu yanamhitaji zaidi katika eneo la ulinzi nadhani atatumika zaidi katika eneo hilo,”alisema kocha huyo.


Yanga baada ya ujio wa Litombo sasa watakuwa na mabeki wa kati wanne ambao ni Bakari Mwamnyeto, Dickson Job na Abdallah Shaibu.


SOMA NA HII  ISHU YA USAJILI YANGA YAPEWA ONYO