Home kimataifa SALAH ATAKA MKWANJA MREFU

SALAH ATAKA MKWANJA MREFU


 MSHAMBULIAJI wa kikosi cha Liverpool, Mohamed Salah amewaambia mabosi zake kuwa anataka kupewa mshahara mnono ili afanye kazi kwa raha akiwa ndani ya kikosi hicho.

Nyota huyo raia wa Misri uwezo wake ni wa hali ya juu na ni miongoni mwa washambuliaji wanaopendwa na mashabiki wa Liverpool pamoja na benchi la ufundi na anatajwa kuwa kwenye rada za timu mbalimbali Ulaya zinazowinda saini yake.

Salah anataka kuwa mchezaji ambaye analipwa mkwanja mrefu zaidi kwenye timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Jurgen Klopp ambaye hivi karibuni alieleza kuwa amefanya mazungumzo na nyota huyo kuhusu kuongeza mkataba mpya.

Kwa sasa kinara anayelipwa mkwanja mrefu ndani ya Liverpool ambayo ni timu kubwa Ulaya ni beki wao wa kati kitasa Virgil van Dijk ambaye analipwa pauni 220,000 kwa wiki na Salah anataka awe anakunja pauni 500,000 kwa wiki.

SOMA NA HII  VIUNGO WAWILI WANATAJWA KUSEPA ARSENAL