Home news SIMBA NA YANGA KUANDIKA REKODI MPYA

SIMBA NA YANGA KUANDIKA REKODI MPYA


UONGOZI wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) umeweka wazi kuwa maandalizi kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Simba v Yanga yamekamilika na matumaini yao makubwa ni kuona kwamba mchezo huo utaandika rekodi mpya ya ubora wa maandalizi yake.

Simba na Yanga zinatarajiwa kukutana Jumamosi ya Septemba 25, katika mchezo wa kukata na shoka utakaochoezwa Uwanja wa Mkapa.

Ikumbukwe kwamba mchezo wa Ngao ya Jamii ni maalumu kwa ajili ya kutoa taarifa kwamba pazia la Ligi Kuu Bara kwa msimu mpya linafunguliwa na ratiba ipo tayari kwa msimu wa 2021/22.

Mkuu wa Idara ya Ligi, Jonathan Kassano amesema kuwa kila kitu kuhusiana na mchezo huo kipo sawa na kinachosubiriwa ni mchezo wenyewe.

“Kila kitu kuhusiana na maandalizi ya mchezo wa Ngao ya Jamii ambao unatarajia kuzikutanisha Simba na Yanga utakaochezwa Uwanja wa Mkapa kimekamilika na kinachosubiriwa niJumamosi ifike utekelezaji wa mchezo huo.

“Kutokana na maandalizi ambayo tumeyafanya mpaka sasa tunaamini kwamba mchezo wa mwaka huu utaweka rekodi ambayo haikuwahi kuandikwa katika maandalizi ya mchezo huo,” amesema.

Chanzo:Championi.

SOMA NA HII  KISA RATIBA YA LIGI KUU...KOCHA MKUU SIMBA AIBUKA HILI JIPYA...AVUNJA UKIMYA KUHUSU MECHI NYINGI ZA 'HOME'....