Home kimataifa SPURS YAMPA HASIRA KEANE

SPURS YAMPA HASIRA KEANE


MCHAMBUZI wa masuala ya michezo, Roy Keane amesema kuwa kwa sasa Klabu ya Tottenham inamshangaza kutokana na kuwa mbovu katika masuala ya kuwa na tamaa ya kusaka ushindi jambo linalompa hasira katika kuitazama.

Jumapili ya Septemba 19, ubao wa Uwanja wa Tottenham Hotspur baada ya dakika 90 ulisoma Tottenham 0-3 Chelsea ilikuwa ni katika mchezo wa Ligi Kuu England.

Wakati Chelsea ikisepa na pointi tatu mazima ilikuwa ni Thiago Silva alipachika bao la kwanza dakika ya 49, N’Golo Kante alipachika bao la pili dakika ya 57 na lile la tatu lilipachikwa na Antonio Rudiger dakika ya 90.

Keane amesema kuwa ameshangazwa na Tottenham kupoteza kwa mabao hayo ikiwa nyumbani jambo ambalo linatokana na kutokuwa na tamaa ya kutaka kufunga.

“Sitaki kuamini kwamba Spurs wamekuwa ni wabaya kiasi hiki. Unaweza ukawa katika siku mbaya na muda mwingine unapoteza ule ubora lakini hawa wamepoteza kabisa tamaa ya kusaka bao.

“Ninajiskia hasira kuitazama Spurs leo. Tofauti katika tamaa ya kusaka ushindi imekuwa ikionekana tofauti wapo chini kabisa, “.

Kwenye Ligi Kuu England kinara ni Chelsea akiwa na pointi 13 huku Spurs ikiwa nafasi ya 7 na ina pointi 9.


SOMA NA HII  DUH...HUYU TAJIRI MPYA WA CHELSEA NAYE 'WALE WALE TU'...KUMBE NAYE ANAPESA ZA' MAWAZO SANA'...