Home news NYOTA FEISAL ATAJWA KUWA HATARI KWA SASA NDANI YA YANGA

NYOTA FEISAL ATAJWA KUWA HATARI KWA SASA NDANI YA YANGA


 ALIYEKUWA Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe amefunguka kuwa kiungo wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ ni mchezaji mzuri na hatari zaidi kwenye kikosi cha Yanga.

Tambwe ambaye aliwahi kuitumikia Yanga na Simba pia kwa nyakati tofauti kwa msimu huu wa 2021/22 anakipiga ndani ya Klabu ya DTB ambayo inashiriki michuano ya Championship ikiwa inatafuta nafasi ya kushiriki ligi kuu msimu ujao.

Nyota huyo kwenye mchezo wa kwanza aliifungia DTB mabao manne dhidi ya Lyon uliochezwa Uwanja wa Uhuru.

Kwenye mchezo huo Tambwe alipiga jumla ya mashuti 7 ambapo manne yalijaa kimiani, moja lilikwenda nje ya lango na mawili yaligonga mwamba.

Akizungumza na Championi Jumatano, Tambwe alisema kuwa: “Kwa kikosi cha Yanga Fei Toto ni mchezaji hatari, niliwahi kucheza nae ila mwanzo alikuwa anacheza namba sita nafasi ambayo ilikuwa inamfanya acheze faulo nyingi ila kwa sasa anacheza namba kumi wamempatia sana kwani ni mchezaji ambaye anapenda kuuchezea mpira.”

Msimu wa 2021/22 Yanga ikiwa imefunga mabao mawili kwenye ligi, Fei ametupia bao moja ambapo aliwatungua Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba.

SOMA NA HII  SAA CHACHE KABLA YA KUSHUKA UWANJANI...PABLO AIBUKA NA JIPYA SIMBA..AFUNGUKA HALI ILIVYO...