Home news SIMBA KUKWEA PIPA KUWAFUATA WABOTSWANA

SIMBA KUKWEA PIPA KUWAFUATA WABOTSWANA


WAWAKILISHI wa Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba wanatarajia kukwea pipa wiki hii kuwafuata wapinzani wao nchini Botswana.


Ni Oktoba 15,2021 jioni wawakilishi hao wanatarajia kukwea pipa ili kuwawahi wapinzani wao Jwaneng Galaxy FC.
Mchezo wao unatarajiwa kuchezwa Oktoba 17 na Simba itaanzia ugenini kisha ule wa marudio unatarajiwa kuchezwa Oktoba 22, Uwanja wa Mkapa.
Kwa mujibu wa uongozi wa Simba umeeleza kuwa Ijumaa ni siku ya timu hiyo kuwafuata wapinzani hao ili kuweza kufanya maandalizi ya mwisho.
Leo Oktoba 12, kikosi kilifanya mazoezi katika Uwanja wa Boko Veteran kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo.

Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema kuwa wanatambua kwamba kila mmoja anatambua kuwa wanakwenda kufanya kazi ngumu na kila mchezaji anajua kinachohitajika.
SOMA NA HII  GAMONDI AIPIGA CHABO SIMBA KWA MKAPA....