Mshambuliaji wa Liverpool, Sadio Mane amekuwa mshambuliaji wa tatu kutoka Afrika kufunga mabao 100 katika historia ya Ligi Kuu ya Uingereza kufuatia jioni ya leo kuisaidia klabu yake kushinda kwa mabao 5-0 dhidi ya Watford wakiwa ugenini.
Salah ambaye alifunga katika mchezo huo, amefikia rekodi ya Didier Drogba ambaye aliichezea Chelsea ambapo alifikisha mabao 104 katika orodha hiyo.
Mohamed Salah amefikisha mabao 8 katika michezo 8 ya mashindano yote mfululizo, na pia amefunga mabao 9 kati ya michezo 10 ya mwisho.
Roberto Firmino raia wa Brazil alifunga mabao matatu peke yake ambapo ni hat trick yake ya kwanza tangu afanye hivyo disemba mwaka 2018.
Ulikuwa mchezo wa kwanza kwa kocha Claudio Ranieri tangu ajiunge na Watford ambao pia wamepokea kipigo kikubwa cha kwanza tangu mwaka 2019 walipochakazwa kwa bao 8-0 dhidi ya Manchester City.
Liverpool wanaongoza Ligi Kuu ya Uingereza wakiwa na alama 18 katika michezo 8 waliyocheza.