news

MORRISON AWAPANIA WABOTSWANA KESHO….ATOA AHADI HII MPYA …

admin October 23, 2021 2:30 pm


STAA wa Simba, Bernard Morrison amesema kuwa mchezo wao wa kesho Jumapili dhidi ya Jwaneng Galaxy atacheza kwa juhudi zaidi ya alivyocheza akiwa Botswana.

Morrison amesema mchezo huu ndiyo utawapa nafasi wao ya kusonga mbele kwenye hatua ya makundi na kama wakizembea hadithi huenda ikawa tofauti.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Morrison alisema kwenye mchezo wa kwanza alijitahidi kwa kadiri alivyoweza ili kuisaidia timu na ikawa hivyo kwa kupata ushindi na sasa wakiwa nyumbani atawavuruga zaidi Waswana hao.

“Mchezo wa kwanza ulikuwa mgumu japo tulishinda, naamini wale watakuwa wametusoma sisi tunachezaje na watakuja na mpango.

Kazi yangu itakuwa moja ambayo ni kucheza kwa juhudi.“Walinichezea hovyo sana nikiwa kwao na nimelijua hilo na sasa itabidi nibadilike mimi pamoja na timu ili tuweze kuwashangaza na kupata ushindi mkubwa zaidi,” alisema Morrison.

PAMOJA NA SAKHO KUANZA KUKIWASHA MSIMBAZI…MECHI YA KESHO ATAISHIA KUITAZAMIA JUKWANI ‘UTAMU’ WA ‘FEI TOTO’ WAMTIA ‘WAZIMU’ NABI…CHUJI ASHINDWA KUJIZUA AFUNGUKA A-Z

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply