News

PAMOJA NA SAKHO KUANZA KUKIWASHA MSIMBAZI…MECHI YA KESHO ATAISHIA KUITAZAMIA JUKWANI

admin October 23, 2021 9:00 am


Kiungo mshambuliaji Pape Ousmane Sakho, amerejea mazoezini pamoja na wachezaji wenzake baada ya kupona jeraha la mguu lililokuwa linamsumbua.

Sakho alipatwa majeraha katika mchezo wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji uliopigwa Uwanja wa Jamhuri mwanzoni mwa mwezi huu.

Pamoja na kuanza mazoezi Sakho bado yupo chini ya uangalizi wa madaktari ili kuhakikisha anapona jeraha lake na kuwa sawa tayari kwa kuanza kucheza tena kwenye mechi mbalimbali za Ligi Kuu na michuano ya Ligi ya Mabingwa.

Hata hivyo, uwezekano wa Sakho kuwepo katika kikosi kitakachocheza mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy Jumapili ni mdogo kutokana na kutokuwa fiti asilimia 100.

WAKATI MECHI YAO DHIDI YA WALIBYA NI LEO..BIASHARA UNITED BADO WAPO TZ…TFF YATUMA BARUA CAF.. MORRISON AWAPANIA WABOTSWANA KESHO….ATOA AHADI HII MPYA …

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply