Home CAF BAADA YA CAF KURUHUSU MASHABIKI…WABOTSWANA WAINGIA HOFU DAR…KOCHA WAO AFUNGUKA

BAADA YA CAF KURUHUSU MASHABIKI…WABOTSWANA WAINGIA HOFU DAR…KOCHA WAO AFUNGUKA


GUMZO lililotawala kwa mashabiki wa Jwaneng Galaxy ya Botswana ni nyomi la mashabiki wa Simba kwenye mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Jumapili jijini Dar es Salaam.

Wengi wao wanahofia Simba inaweza kujaza mashabiki 60,000 Uwanja wa Mkapa na kuipa timu yao kipigo kizito kuliko kile cha mabao 2-0 nchini Botswana.

Lakini, Kocha Morena Ramoreboli amesikia maneno hayo na kujibu kwa kiburi kuwa hawahofii chochote kwani hawaji kucheza na mashabiki bali na wachezaji 11.

“Ilibidi kufanya mabadiliko haraka wachezaji waingie kuzoea mchezo na kubadili matokeo, lakini ikashindikana. Wikiendi hii tunakwenda na mkakati wa tofauti ugenini,” alisema. “Changamoto ya mashabiki 60,000 haiwezi kutuzuia kuweka sawa mipango. Tunakwenda kucheza kwa kujiamini na juhudi kubwa. Kama tukienda na hofu ya mashabiki hatutafanikiwa. Hatuendi pale kuhangaika na mambo ya mashabiki wao, tutapambana.”

Simba haina rekodi ya kupoteza mchezo muhimu wa michuano hiyo hivi karibuni kwenye uwanja huo tena ikiwa imeshinda kwa idadi kubwa ya mabao ugenini.

Kocha wa Simba, Didier Gomes ametamba kuwa mechi ya kwanza walilazimika kwenda na lengo la kusaka pointi kisha Dar es Salaam ndiko watakakoonyesha ufundi.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA TAARIFA ZAKE ZA KUWA MAJERUHI ZIPO NYINGI..CHICO AIBUKA NA KUVUNJA UKIMYA..