Home news BEKI SIMBA ASHONWA NYUZI SITA,MACHOZI NA MAUMIVU YAKUTOSHA

BEKI SIMBA ASHONWA NYUZI SITA,MACHOZI NA MAUMIVU YAKUTOSHA


 BEKI wa kati wa Simba, Kennedy Juma, ameshonwa nyuzi sita baada ya kupata jeraha kubwa kwenye eneo la jicho kutokana na kuumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji.

Kennedy alijikuta anaondolewa na machela kwenye uwanja dakika ya 43 ya mchezo huo kufuatia kupigwa na kiwiko na straika wa Dodoma, Anuar Jabir, ambaye naye alilimwa kadi nyekundu.

Mtu wa karibu na daktari wa Simba, Yassin Gembe, aliliambia Championi Jumatatu kuwa hali ya Kennedy inazidi kutengemaa na ameshonwa nyuzi sita jirani na jicho na kwa sasa anaendelea kuimarika.

“Kennedy jicho lilivimba kabisa, ile ilikuwa ni rafu mbaya sana ambayo alichezewa na yule mchezaji wa Dodoma, ililazimika ashonwe nyuzi sita ili kuweza kukaa sawa,” alisema mtu huyo.

Mtu huyo aliongeza kuwa Kennedy alilia na kusikitika sana baada ya kupata majeraha hayo kwa sababu alijua nafasi yake ya kwenda kambi ya timu ya Taifa imeingia mchanga.

“Kennedy alilia na kuumia sana moyoni kwa sababu hiki ndiyo kipindi ambacho alikuwa anaaminiwa timu ya Taifa Stars, sasa maumivu yake yalikuwa makubwa,”.

Tayari nyota huyo kwa sasa anaendelea vizuri na alikuwa moja ya wachezaji wa Stars ambao walianza jana mazoezi na timu ya taifa ya Tanzania, Uwanja wa Mkapa.


SOMA NA HII  SIMBA SC WAPANGUA JANJA YA WYDAD KUTAKA KUSHITAKI CAF ENDAPO WATAFUNGWA LEO...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here