Home Burudani DULLA MBABE APOTEZA KWA POINTI

DULLA MBABE APOTEZA KWA POINTI


BONDIA Mtanzania, Dulla Mbabe amepoteza katika pambano lililopewa Kiboko ya Wageni katika pambano la raundi 10 mbele ya Tshimanga Katompa usiku wa kuamikia leo.

Pambano hilo lilikuwa na ushindani mkubwa ilishuhudiwa vitasa vya maana kutoka kwa mabondia hao wawili huku Mbabe akishindwa kuonyesha ubabe.

Katompa raia wa DR Congo alionekana kuzijua mbinu za Mbabe ambapo makonde aliyokuwa anamshushia yalikuwa na ujazo mzito kwelikweli.

Ni ushindi wa pointi ambao Katompa amepata mbele ya mfalme wa Wazaramo, Dulla Mbabe.

Pambano hilo la kukata na shoka lilifanyika katika ukumbi wa PTA Sababasaba na ilikuwa mubashara ndani ya Azam TV.

Inakuwa ni pambano la pili kwa Mbabe kubwa kupoteza kwa kuwa alikuwa ametoka kupoteza lile alilotwangana na Twaha Kiduku.

SOMA NA HII  YANGA KUMLETA CHID BENZ VS MADEAMA