Home news KISA MECHI NA AZAM…UONGOZI YANGA WAACHUKUA MAAMUZI MAGUMU…WACHEZAJI WATAJWA

KISA MECHI NA AZAM…UONGOZI YANGA WAACHUKUA MAAMUZI MAGUMU…WACHEZAJI WATAJWA

 


YANGA wana jambo lao. Mashabiki wa Arusha watanuna lakini wale wa Dar es Salaam na mikoa ya jirani watafurahia.

Yanga wameamua kurejesha mechi yake na Azam Jijini Dar es Salaam tofauti na awali ilivyokuwa imepangwa kupigwa Arusha.

Gazeti la Mwanaspoti limebaini kwamba Yanga wamefikia uamuzi wa mechi hiyo ya Oktoba 30 irudishwe kwenye Uwanja wa Mkapa.

Mmoja wa viongozi wa Yanga ameliambia gazeti la Mwanaspoti kwamba wameamua kurejesha mechi hiyo Dar es Salaam kimkakati kwavile ni moja ya turufu kubwa ya ubingwa wa Tanzania msimu huu. Habari za ndani ya uongozi zinasema kwamba, Yanga machale yamewacheza kwamba wakikomaa mechi hiyo ipigwe Arusha wataambulia majeruhi lakini wanaweza kukumbana na habati mbaya kwenye matokeo na wakaathirika kuelekea katika azma yao ya ubingwa.

Uongozi umejiridhisha kwamba uwanja Sheikh Abeid si salama kwa sasa kwa mastaa wake haswa kwenye eneo la kuchezea.

Mmoja wa viongozi wa Yanga aliliambia gazeti Mwanaspoti wameona waendelee kuutumia uwanja wa Benjamin Mkapa baada ya kuona hali ya uwanja wa Arusha sio nzuri ikiwa ni mwanzoni mwa Ligi na kama watalazimisha watapata pancha nyingi ambazo huenda zikawaathiri siku zijazo.

“Tumeona bora tucheze palepale kwa Mkapa kwa sababu tunaweza tukacheza Arusha lakini sasa wachezaji wetu wakapata majeraha, tulikuwa na lengo la kuwapa burudani pia mashabiki wetu wa kule pamoja na kuongeza mapato kwa mauzo ya jezi lakini sasa hakuna namna,” alidokeza mmoja wa viongozi wa Yanga.

Alipotafutwa ofisa habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alikiri mchezo utarejeshwa katika Uwanja wa Mkapa lakini hakuwa tayari kufafanua sababu.

“Kweli mchezo utachezwa hapa hapa kwa Mkapa, siwezi kusema sababu ni nini ila we elewa hivyo,” alisema kwa kifupi Bumbuli huku kanuni zikiiruhusu timu kuchagua mchezo mmoja wa kuchezwa nje ya uwanja wake wa nyumbani kwa msimu husika.

Yanga kwasasa wanaendelea na mazoezi katika uwanja wao wa Avic Town kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya KMC utakaopigwa Oktoba 19 katika uwanja wa Majimaji, Songea.

SOMA NA HII  HII HAPA MASHINE YA MAGOLI YA MARUMO ILIYOWAINGIZA VITANI MABOSI WA SIMBA NA YANGA...

Baada ya mchezo huo Yanga watarejea tena jijini Dar es Salaam na kuendelea na mazoezi katika uwanja wao wa Avic Town wakijiandaa na mchezo dhidi ya Azam utakaopigwa saa 1:00 usiku katika uwanja wa Benjamin Mkapa.