Home news MASHABIKI YANGA WAITWA KWA MKAPA KUSHUHUDIA PIRA PASI

MASHABIKI YANGA WAITWA KWA MKAPA KUSHUHUDIA PIRA PASI


UKIWA na buku tatu tu kwa mwanafamilia ya michezo unaweza kuuona ule uwezo wa kiungo mwenye jukumu la kugawa pasi za upendo Dickson Ambundo pamoja na nyota wengine ambao hawajaitwa kwenye timu zao za taifa.

Yanga wamewaita mashabiki wao Uwanja wa Mkapa ili waweze kushuhudia pira pasi ndani ya dakika 90 kama ambavyo wamekuwa wakifanya hivyo kwenye mechi zao za ligi.

Leo Yanga inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya JKU SC mchezo ambao unatarajiwa kuanza saa 1:00 usiku, Uwanja wa Mkapa.

Awali mchezo huo ulitarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex ila taarifa iliyotolewa na Yanga imeeleza kuwa utachezwa Uwanja wa Mkapa.

Mbali na  kiingilio cha 3,000 kwa mzunguko, eneo lile laVIP B&C itakuwa ni 5,000  na 10,000 VIP A.

Wachezaji wengine ambao wanatarajiwa kuwepo leo ni pamoja na Abdalah Shaibu, Farid Mussa, Bangala Litombo, Paul Godfrey.



SOMA NA HII  PAMOJA NA KUKABILIWA NA CAF SUPER LEAGUE...SIMBA WARUHUSU MASTAA WAKE KUMWAGILIA MOYO...