Home Habari za michezo BAADA YA KUSUASUA KATIKA MICHEZO YA CAFCL MGUNDA AWAPA NENO HILI MASHABIKI

BAADA YA KUSUASUA KATIKA MICHEZO YA CAFCL MGUNDA AWAPA NENO HILI MASHABIKI

MGUNDA SIMBA TUNAUTAKA UBINGWA LIGI KUU...

MKURUGENZI wa ufundi  wa Simba, Juma Mgunda amewataka mashabiki wa timu hiyo kuwa wamoja na kuwapa ushirikiano viongozi wao hasa katika kipindi hiki cha mpito.

Amesema Simba imepita katika kipindi cha mpito na sasa mwanga unaonekana na anaimani kubwa ya timu hiyo kufikia malengo yao ya kucheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kutwaa mataji ya Ligi Kuu Tanzania Bara na FA.

Mgunda amesema anaifahamu vizuri Simba na yaliyopita yalikuwa ni kipindi cha mpito na sasa timu yao imeanza kusimama na kurejea kama ilivyokuwa awali.

Ameeleza  mashabiki wawe na imani na viongozi, benchi la ufundi pamona na wachezaji wao kwa sababu ninaimani kubwa ya kufanya vizuri katika michezo iliyopo mbele yao hasa mechi zilizosalia za hatua ya robo fainali ya ligi ya Mabingwa.

“Ninaimani na Simba yaliyopita ilikuwa kipindi cha mpito, lakini sasa timu imeanza kurejea katika ubora wake  kama ilivyokuwa awali, kikubwa mashabiki wanatakiwa kusapoti timu yao na kuendeleza kauli mbiu yetu ya Nguvu mmoja,” alisema Mgunda.

Ameongeza kuwa hapa presha kabisa na Kocha Mkuu Abdelhak Benchikha aliyekuwepo sasa ndani ya kikosi cha Simba kwa sababu kuna mabadiliko yameonekana na kuendelea kufanya vizuri.

Kuhusu usajali wa dirisha dogo, Mgunda amewataka mashabiki kutokuwa na presha muda utakapofika kila kitu kitawekwa wazi na kuoba maboresho ya kikosi chao kwa kufuata mapendekezo ya benchi la ufundi kulingana na mahitaji ya timu hiyo.

SOMA NA HII  MSIMAMO WA LIGI KUU TANZANIA BARA UPO NAMNA HII