Home Habari za michezo SERIKALI YAAMUA KUFANYA KWELI KWA WAAMUZI…YASIKIA KILIO CHA SIMBA NA YANGA KUHUSU...

SERIKALI YAAMUA KUFANYA KWELI KWA WAAMUZI…YASIKIA KILIO CHA SIMBA NA YANGA KUHUSU HAKI…


Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Serikali imejipanga kuwafadhili Waamuzi kwa kuwapeleka nje ya Nchi kupata mafunzo yatakayowaimirisha kujua vyema Sheria na Utaratibu wa Soka.

Waziri Mchengerwa pia amesema Serikali itaendeleza Elimu ya Uraia na Uzalendo kwa taifa letu ili kuondokana na vitendo vya rushwa na upendeleo michezoni vitu ambavyo ni kinyume na Maadili nchini.

”Licha ya kuwa TFF imekuwa ikiandaa semina mbalimbali na hata kuwafungia waamuzi takribani 13,sisi Serikali tumeandaa mpango kazi kupitia asilimia 5 ambayo Mh. Rais ameitenga kupitia bajeti ya mwaka jana2021/2022 ambayo moja kwa moja itakwenda kutengeneza waamuzi wapya” aemsema Waziri Mchengerwa.

”Serikali tumejipanga kuhakikisha kwamba tunawafadhili Waamuzi wapya ambao watakwenda kusoma kama itakuwa ndani ya nchi kwenye chuo chetu cha Mallya tunachokijenga na Mh Rais wa nchi ametoa fedha za kutosha,lakini pia wapo Waamuzi tutawapeleka nje ya nchi kwenda kujifunza itakayowawezesha kuwa waamuzi wazuri watakaojua vyema sheria na taratibu lakini pia kuendeleza elimu ya uraia na uzalendo kwa taifa letu ili kuondokana na vitendo vya rushwa,upendeleo vitendo vilivyo kinyume na maadili” alimalizia Waziri mwenye dhamana ya Michezo, Mchengerwa. 

Endapo kweli jambo hili litafanyika, itakuwa ni sawa na Serikali kusikia kilio cha klabu nyingi za Ligi Kuu, ikiwemo Simba na Yanga ambapo mara nyingi zimekuwa zikilia haki kutokana na waamuzi mbalimbali kushindwa kutafsiri sheria za soka pindi wanapozichezesha kwenye mechi za Ligi.

SOMA NA HII  BAADA YA KUWATAZAMA SIMBA WANAVYOCHEZA...PATRICK PHIRI KAGUNA KISHA AKAWASHTUA MABOSI MSIMBAZI KWA HILI...