Home Uncategorized SINGIDA UNITED YAIPA SOMO LA KUTOSHA DODOMA FC

SINGIDA UNITED YAIPA SOMO LA KUTOSHA DODOMA FC

MBWANA Makatta, Kocha Mkuu wa Dodoma FC ambayo imeshashika mkononi tiketi ya kushiriki Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21 amesema kuwa wamejifunza kupitia kuporomoka kwa Singida United ambayo itashiriki Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao.
Singida United ambayo ilipanda ligi msimu wa 2017/18 ma kumaliza ligi ikiwa nafasi ya tano kwa sasa inashika nafasi ya 20 ikiwa na pointi 18 baada ya kucheza mechi 37.
Akizungumza na Saleh Jembe, Makatta amesema kuwa anatambua ugumu ndani ya ligi na kilichowashinda Singida United ni darasa kubwa kwao msimu ujao.
“Hakuna ambaye hakuwa akiona ushindani wa Singida United ndani ya uwanja ila kilichowakwamisha ni upande wa uchumi pamoja na wachezaji kutopewa stahiki zao, nina amini ni darasa tosha kwangu msimu ujao.
“Ninaamini katika kazi yangu pamoja na wachezaji nilionao hivyo kazi kubwa ipo na kila mchezaji yupo tayari huku tukipewa sapoti kubwa kutoka kwa uongozi,” alisema.
  Dodoma FC pia wana taji la jumla la mshindi wa timu ya Ligi Daraja la Kwanza ambapo waliinyoosha Gwambia FC bao 1-0, mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

SOMA NA HII  YANGA YAGONGANA NA AZAM FC ZAKUTANA KWA KIPA WA KAGERA SUGAR KUSAKA SAINI YAKE