Home Uncategorized SIMBA YAZITAKA POINTI TATU ZA COASTAL UNION LEO, MKWAKWANI

SIMBA YAZITAKA POINTI TATU ZA COASTAL UNION LEO, MKWAKWANI


UONGOZI wa Simba umesema kuwa unahitaji pointi tatu leo kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Coastal Union utakaopigwa majira ya saa 10:00 jioni.

Simba inakutana na Coastal Union inayonolewa na Juma Mgunda, Uwanja wa Mkwakwani,Tanga.

Mchezo wao wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa, Simba ilishinda mabao 2-0 ambayo yalifungwa na Gerson Fraga.

Timu zote hazina presha ya kushuka daraja kwa kuwa zina uhakika wa kubaki kwa msimu ujao wa 2020/21.

Simba ambao ni mabingwa wa ligi wapo nafasi ya kwanza na pointi 84 huku Coastal union ikiwa nafasi ya saba na pointi 52.

Akizungumza na Saleh Jembe, Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa kila kitu kipo sawa na wachezaji wanatambua majukumu yao.

“Tunawaheshimu wapinzani wetu Coastal Union ila tunahitaji pointi tatu ili kujiweka sawa kwa ajili ya mchezo wetu ujao dhidi ya Polisi Tanzania.

“Utakuwa ni mchezo mgumu kwa kuwa tunacheza na timu nzuri hivyo mashabiki wajitokeze kutupa sapoti,” amesema.

SOMA NA HII  UONGOZI YANGA WASHINDWA KUJIZUIA, WASHUSA RUNGU KWA MASHABIKI WAKE