Home kimataifa NYOTA RICE DAU LAKE NOMA,MANCHESTER UNITED WAAMBIWA WAMCHUKUE

NYOTA RICE DAU LAKE NOMA,MANCHESTER UNITED WAAMBIWA WAMCHUKUE

 MABOSI wa Manchester United wameambiwa kuwa itakuwa vema kwao ikiwa watapambana kupata saini ya kiungo anayekipiga ndani ya Klabu ya West Ham United,  Declan Rice.

Neno hilo limetoka kwa nyota wazamani wa Arsenal wengi wanapenda kuwaita washika bunduki Nigel Winterburn ambaye amesema kuwa itakuwa sahihi  ikiwa Manchester United watafanikiwa kupata saini ya nyota huyo.

Rice amekuwa akiwindwa na timu nyingi za Ulaya ikiwa ni pamoja na Manchester United, Manchester City pamoja na Chelsea ambazo zote zinashiriki Ligi Kuu England. 

Dau la kuipata saini ya kiungo huyo kutokana na ubora wake ndani ya uwanja linatajwa kuwa ni pauni milioni 90 jambo ambalo Nigel anaona kuwa itakuwa ni faida kwa United. 

“Pauni 90 m ni fedha nyingi sana kwa ajili ya Declan Rice inashangaza ila huenda ni dau lake na atakuwa msaada kwa timu kama watampata,”.

SOMA NA HII  MO SALAH ATUPIA MAWILI WAKATI TIMU YAKE IKISEPA NA POINTI TATU MBELE YA WEST HAM UNITED