Home news WANACHOKITAKA MASTAA YANGA NI HIKI HAPA MBALI NA MKWANJA

WANACHOKITAKA MASTAA YANGA NI HIKI HAPA MBALI NA MKWANJA


 ACHANA na bonasi za kila mechi wanazozipata kutoka kwa wadhamini wao kampuni ya GSM imefichuka kuwa kitu kikubwa ambacho kinawapa motisha ya kufanya vizuri mastaa wa Yanga, ni malengo ya kutaka kuandika rekodi ya kushinda ubingwa wa Ligi Kuu Bara baada ya kupita misimu minne.

Yanga imeuanza kwa kasi msimu huu wa 2021/22 kwa kushinda taji la Ngao ya Jamii na kuvuna pointi sita katika michezo yao miwili ya kwanza, huku wakiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara mpaka sasa.

 Mara ya mwisho Yanga kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara ilikuwa msimu wa 2016/17, na baada ya hapo Simba walitwaa taji hilo mara nne mfululizo.

Akizungumza na Championi Jumatatu, aliyekuwa Kaimu Katibu Mkuu ambaye sasa ni Mkurugenzi wa fedha wa Yanga, Haji Mfikirwa alisema: “Miongoni mwa sera za klabu yetu katika kuwapa motisha wachezaji ni kuhakikisha kunakuwepo na kiwango fulani cha bonasi kwa kila matokeo mazuri wanayoyapata.

“Lakini nikuhakikishie kuwa hicho siyo kitu pekee kinachowapa motisha kuna jambo ambalo wanahitaji kulifanya na wanapambana kwa sasa.


“Motisha kubwa ambayo wachezaji wote wa Yanga wanayo msimu huu ni ile ya kutaka kuandika rekodi ya kuwa sehemu ya kikosi kitakachorejesha ubingwa wa Ligi Kuu Bara baada ya kupita misimu minne mfululizo bila taji hilo, kila mchezaji anatamani kuona hilo linatimia ndiyo maana wanapambana kufanya vizuri.”


SOMA NA HII  MIEZI KADHAA BAADA YA KUACHANA NA YANGA...NTIBAZONKIZA AVUNJA UKIMYA...AIBUKA NA HAYA MAPYA...