Home news YANGA WATAMBA KUONGEZA MAKALI YA FISTON MAYELE, MAKAMBO

YANGA WATAMBA KUONGEZA MAKALI YA FISTON MAYELE, MAKAMBO


 KOCHA Msaidizi wa Yanga, Mrundi, Cedric Kaze, amesema siku 15 za kambi ya mkoani Arusha watazitumia kutengeneza muunganiko katika safu yao ya ushambuliaji.

Kauli hiyo ameitoa ikiwa ni siku chache tangu timu hiyo itoke kucheza mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Geita Gold uliochezwa wiki iliyopita na Yanga kushinda 1-0, mfungaji akiwa Jesus Moloko.

Timu hiyo inatarajiwa kusafiri kuelekea Arusha kwa ajili ya kambi fupi kupisha michezo ya timu ya timu za taifa.

Akizingumza na Spoti Xtra, Kaze alisema anaamini watakaporejea katika ligi watakuwa imara zaidi na kuendelea na kasi yao ya ushindi.

Kaze alisema kuwa, wamepanga kutumia siku 15 kwa ajili ya kambi mkoani huko, kikubwa wataziboresha sehemu zote zenye upungufu ili kuhakikisha wanafikia malengo waliyojiweka ya kupata ushindi katika kila mchezo.

Aliongeza kuwa sehemu watakayoanza nayo kuifanyia kazi ni ushambuliaji ambayo inashindwa kutumia nafasi nyingi za kufunga mabao ambayo inaongozwa na Fiston Mayele, Heritier Makambo na Yusuph Athumani.

β€œMechi mbili tumepata ushindi na kukusanya pointi sita, licha ya kuendelea kuimarika katika baadhi ya nafasi katika timu yetu ya Yanga, lakini tatizo lililopo ni kwenye ushambuliaji ambapo benchi la ufundi tumepanga kulifanyia kazi kwa siku 15 tutakazokaa Arusha.

β€œKikubwa mashabiki waendelee kutusapoti ili kuhakikisha tunafanikisha malengo yetu ya msimu ya kubeba ubingwa wa ligi,” alisema Kaze.


SOMA NA HII  FT: SIMBA WAIFUATA YANGA KIBABE....PHIRI KAMA KAWA....ONANA MHHHH.....!!!!