Home Uncategorized KUMBE HII NDIO SUPRISE YA SIMBA, MONDI APIGA SHOW MOJA MATATA KWA...

KUMBE HII NDIO SUPRISE YA SIMBA, MONDI APIGA SHOW MOJA MATATA KWA MKAPA


 MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Nasib Abdul, Diamod leo Agosti 22 ameweka rekodi yake kwa kutumbuiza mbele ya mashabiki wa Simba ambao walijitokeza kwa wingi Uwanja wa Mkapa kwenye kilele cha Simba day.


Diamond alitua Uwanja wa Mkapa akiambatana na Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara kwa Helkopta jambo lililozua shangwe kwa mashabiki mwanzo mwisho.


Baada ya kushuka Mondi alianza kutoa burudani moja kwa moja bila kusubiri kuitwa na MC Mpoki kama ilivyokuwa kwa Meja Kunta na  Mario ambao nao walitumbuiza kwenye tamasha hilo.


Wimbo mpya wa Simba aliurudia mara mbili huku mashabiki wakimshangilia nyota huyo mwenye uwezo wa kuimba na kucheza.


Katika harakati za kucheza Mondi, shabiki mmoja ambaye hakufahamika jina lake alimrukia Mondi na kumkubatia jambo lililozua tafrani kidogo kabla ya shabiki huyo kuondolewa na Polisi pamoja na mabausa wa Mondi.


Licha ya Mondi naye kuanguka alijifuta na kuendelea kupiga show baada ya kumaliza alisepa kwa kukwea Helkopta na kumuacha Manara akiendelea na shughuli za kuwatambulisha wachezaji wapya na wazamani wa Simba kwenye kilele cha Simba day.

 Inaelezwa kuwa ‘Surprise’ ambayo ilikuwa ikisemwa na Manara awali kabla ya kilele cha Simba day ilikuwa ni burudani kwa mashabiki wake kutoka kwa wasanii wa Bongo pamoja mtindo wa kutoa kwa Manara na Mondi kwa kutumia Helkopta.

SOMA NA HII  BORUSSIA DORTMUND WAIGANDA SAINI YA SANCHO