KLABU ya Simba imekiri kuwa tangu Ligi Kuu Tanzania Bara imeanza kikosi hicho kinapitia wakati mgumu kwani wanacheza kwa presha kubwa ili kuhakikisha wanapata matokeo lakini mambo bado sio mazuri kwa upande wao.
Hayo yamesemwa jana Jumanne, Novemba 2, 2021 na Kocha Msaidizi wa Simba, Selemani Matola wakati akizungumza na wanahabari kuelekea mchezo wao wa leo dhidi ya Namungo FC.
“Ni kweli tunapitia kipindi kigumu, timu inacheza kwa presha ndiyo maana tunapoteza nafasi nyingi za kufunga. Tunapata muda mdogo wa kufanya marekebisho mapungufu kutokana na mechi kuwa karibu karibu.
“Kikosi kipo vizuri kwa mechi ya kesho{leo}. Namungo wana timu nzuri, tunawaheshimu kwa hilo lakini na sisi tumejipanga kupata matokeo mazuri,” amesema Matola.
Aidha, Matola amethibitisha wachezaji wafuatao watakosa mchezo wa kesho dhidi ya Namungo Fc kutokana na majeraha.
1. Ousmane Sakho
2. Taddeo Lwanga
3. Mzamiru Yassin
4. Chris Mugalu.
Kwa mechi nne za Ligi, Simba wameshinda mechi mbili, wametoa sare mehi mbili, wamefunga mabao mawili tofauti na misimu minne iliyopita.