Habari za Simba
Habari za michezo

KWASASA SIMBA NI USHINDI TU NA SIVINGINEVYO

Staff Desk September 15, 2023 11:17 am

Mshambuliaji wa Klabu ya Simba, Moses Phiri amesema malengo yao ni kushinda mchezo wa Jumamosi dhidi ya Power Dynamos ya nyumbani kwao Zambia

Phiri ambaye ameondoka na kikosi cha Simba leo kuelekea Zambia kwa ajili ya mchezo huo, amewatoa hofu mashabiki wa Simba kuwa yeye pamoja na wachezaji wenzake wataenda kujituma kwa ajili ya matokeo mazuri

“Tunajua utakuwa mchezo mgumu kwetu kwa sababu watakuwa nyumbani lakini malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda.

“Uzuri ni kwamba ninakwenda kucheza kwenye mazingira ya nyumbani ambako nimekulia, lugha yao wanayozungumza ninaijua, kwa hiyo kwa namna moja au nyingine kutakuwa na urahisi.

“Niwatoe hofu mashabiki, Simba tunakwenda kupambana na sisi kama wachezaji hatuna jambo jingine zaidi ya kutaka ushindi,” amesema Phiri.

KIKOSI CHA SIMBA KIMESHATUA ZAMBIA KIBOSI MAXI AWEKA WAZI HESABU HIZI ZA YANGA KWA AL MAREIKH

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply