Home Makala JINSI VITENDO VYA ‘KISHOGA’ VINAVYOZIDI KUSHAMIRI KWENYE LIGI KUU..WACHEZAJI , VIONGOZI WATAJWA…

JINSI VITENDO VYA ‘KISHOGA’ VINAVYOZIDI KUSHAMIRI KWENYE LIGI KUU..WACHEZAJI , VIONGOZI WATAJWA…

JANA asubuhi katika hali isiyotarajiwa kwenye mitandao ya kijamii, na kwenye magroup ya Whatsapp ya kimichezo kulizuka gumzo kubwa la siku, ambapo video na picha za kijana wa kiume akiwa mtupu akionyesha sehemu zake za nyuma zilijadiliwa na wapenzi wa soka .

Picha hizo zisizo za kimaadili ya kitanzania , zilisambaa kwenye mitandao hiyo huku mtandao wa instagram kupitia watu maarufu mbalimbali wakijaribu kuzitolea ufafanuzi na kwa kujaribu kuhusisha picha hizo na golikipa wa timu kubwa hapa nchini.

Hali hiyo ilizidi kuwa kubwa na kuzua taharuki mpaka kupelekea mchezaji huyo kufuta ukurasa wake wa Instagram ambapo inadaiwa ni kutokana na maneno makali aliyokuwa akitumiwa.

Soka la Bongo lilifanikiwa kufanya mahojiano na watu mbalimbali wakiwemo wadau wa soka na wachezaji wa Ligi Kuu na Championship ambapo mbali na kutoa sababu mbalimbali walisikitika juu ya tukio hilo na kutoa wito kwa jamii ichukue hatua kuzuia matukio kama haya kwani yanaleta aibu katika mchezo wa soka.

Akizungumza kwa sharti la kutoyajwa jina lake, mmoja ya wachezaji wa Ligi Kuu alisema kuwa ni tabia ambayo haivumiliki na inatia aibu mchezo wa soka ambao unatajwa kuwa ni mchezo wenye hadhi na heshima yake hapa nchini.

Mchezaji huyo amesema kuwa vitendo vinavyoashiria ‘Ushoga’ kwenye mchezo wa soka havipaswi kupewa nafasi ya kushamiri kwani vitapelekea taifa kukosa wachezaji mahari kwa ajili ya kulipambania taifa.

Aidha kwa uchunguzi usio rasmi uliofanywa na Soka la Bongo , imebinika kuwa matendo ya ‘Ushoga’ kwa wachezaji wa Ligi Kuu na Ligi za madaraja mengine kwa siku za hivi karibuni yameshamiri ambapo inadaiwa vinatumika kama kigezo cha mchezaji kusajiliwa na timu fulani au kupata nafasi ya kucheza.

Inasemekana kuwa , si tu wachezaji, bali hata viongozi wa klabu na makocha ni wahusika wakubwa wa matendo haya ambayo yanapelekea wachezaji waliofanyiwa vitendo hivi kuishi maisha ya kukosa amani na furaha wakiwa na wasiwasi taarifa zao kujulikana.

Aidha wahanga zaidi wamatendo ya kunajisiwa kimwili, ni wachezaji ambapo mara nyingi makocha na viongozi huwataka kwa lazima aidha wawaingile au waingiliwe wao kinyume na maumbile.

Pia, wachezaji wa timu za vijana na academy nao ni wahanga wa matukio haya ambapo wengi wao inasemakana wamekuwa wakiingiliwa na makocha wao ili wapate nafasi ya kucheza.

Utafiti wetu ulienda mbali zaidi na kubaini hata baadhi ya wachezaji wenyewe kwa wenyewe wamekuwa wakishiriki michezo hiyo kwa kuingiliana wenyewe kwa wenyewe.

Kupitia uchunguzi wetu pia tulibaini kuwa , kuna watu mashuhuri nchini ambao nao pia wamekuwa wakiwawinda wachezaji na kuwataka washiriki nao vitendo hivyo viovu.

Mathalani, inafahamika baadhi ya  wachezaji wa Klabu moja kubwa kutoka mkoani , kwa nyakati tofauti wanapokuwa Dar es salaam, kwenye moja ya hoteli iliyopo Magomeni wamekuwa wakishirki matendo hayo na vijana ‘mashoga’ ndani ya hoteli hio.

SOMA NA HII  WAWAKILISHI WETU KIMATAIFA WAJIPANGE SAWASAWA

Chanzo kinasema wachezaji hao wamekuwa wakihongwa Bangi na pombe kali na ‘mashoga’ hao ili wawafanye kinyume.

Hali kama hii pia inaelezwa kwa wachezaji wa timu ya Halmashauri moja maarufu nchini, pamoja na wachezaji wa timu za Kariakoo.

Kupitia utafiti wetu usio rasmi, tulibaini kuwa wachezaji wengi wa mpira wanashawishika kufanya vitendo hivi kutokana na pesa wanazopewa na ‘mashoga’ mbalimbali ambao wanawataka kimapenzi.

Miaka ya hivi karibuni , mtandao wa Jamii Forum , ilichapishwa taarifa za mchezaji wa zamani wa Simba akidaiwa kushiriki matendo haya.,wachangiaji kwenye mtandao huo waliweka shuhuda zao na kuanika namna wachezaji wa mpira na makocha wanavyoshirki michezo hio.

Hali hii pia ipo kwenye timu za wanawake, ambapo inaarifiwa kuwa baadhi yao wanashiriki vitendo vya kusagana wao kwa wao.

Jambo hili limekuwa kwa muda mrefu likijadiliwa chini ,lakini linamzizi mkubwa kwani vitendo hivi vimeshamiri na imekuwa kama ‘fasheni’ kwa wachezaji hao.

Kwa kuzingatia miiko na maadili ya kitanzani na Afrika kwa ujumla, Soka la Bongo tunatoa wito kwa jamii, wadau na viongozi wa soka na waserikali kuingilia kati kwa kutoa elimu juu ya athari za matukio haya ili kuilinda jamii dhidi ya matendo haya ambayo yanaweza kutia doa jitihada kubwa za kukuza mchezo wa soka.

Aidha, Klabu za soka zijiimarishe kwenye ufuatiliaji ili kuwabaini wachezaji wenye vitendo hivi na kuwasaidia kisaikolojia kuachana na matendo haya.

Pia, Vyombo vya dola viwachukulie hatua kali za kisheria Viongozi na makocha ambao wamekuwa wakiwataka wachezaji kushirkia nao kimapenzi kama rushwa ya kusajiliwa au kupata nafasi ya kucheza.

Tunatoa wito kwa Viongozi wa dini kuisaidia jamii hii kwa kutoa elimu ya dini ili kuimarisha jamii kiimani kwani matendo haya yameshamiri nchini, 

Wito kwa wachezaji, ninyi ni wahanga wa matukio haya mnapaswa mpaze sauti zenu kukomesha tabia hizi chafu ambazo zitaharibu taswira nzuri ilijengwa kuhusu mchezo huu, msikubali kuingia kwenye mtego wa aina yeyote ya kuwapelekea kujitia nuksi na laana ya kushiriki matendo haya ya kifedhuli na aiabu kwenu.

Wafikisheni kwenye sehemu husika wote wanaojaribu kuwataka kushiriki kwenye matendo haya, iwe ni viongozi, makocha au watu mashuhuri.

Pamoja na haya, Soka la Bongo tunaamini katika uhuru wa mtu , na haki zake za faragha zinazozingatia sheria, miiko na maadili ya kitanzania pamoja na Utu, lakini pia tunapinga vikali mambo ya faragha kuanikwa hadharani kwa njia yeyote ile ambayo itapelekea uvunjifu wa maadili.

Tuandikie maoni yako chini kujua mtazamo wako kuhusu vitendo hivi na njia ya kupambana navyo.