Home news BAADA YA KUWA NNJE YA UWANJA KWA MIAKA MIWILI…BALAMA MAPINDUZI AANZA ‘KUCHANGANYA’

BAADA YA KUWA NNJE YA UWANJA KWA MIAKA MIWILI…BALAMA MAPINDUZI AANZA ‘KUCHANGANYA’


Habari njema kwa Yanga ni kwamba hatimaye kiungo wao, Mapinduzi Balama ameshiriki kwa mara mazoezi na kikosi kizima baada ya takribani miaka miwili tangu aumie.

Balama ameshiriki mazoezi hayo juzi na kuonyesha matumaini mapya katika kurejea kwake katika kikosi hicho huku makocha wake wakigundua kitu kimoja.

Akizungumza  jana, kocha wa viungo wa Yanga, Helmy Gueldich alisema kiungo huyo alifanya mazoezi hayo vizuri kwa masaa mawili akiwa na kikosi kizima cha timu hiyo inayongoza msimamo wa ligi.

“Kila mtu amefarijika kumuona (Balama) akicheza jana (juzi) kwa muda sasa alikuwa akifanya mazoezi maalum katika programu aliyokuwa anapewa, lakini sasa ameanza mazoezi na timu nzima,” alisema Helmy.

“Wengi tulisubiri kuona hili nadhani daktari Youssef (Mohamed) amefanya kazi nzuri ambayo sasa itamfanya Balama kurejea kuitumikia klabu kwa wakati mwingine,” alisema.

Balama aliumia takribani mwishoni mwa msimu wa 2019/20 (Juni 2020), wakati akiwa mazoezini, akivunjika kifundo cha mguu wa kushoto na kulazimika kufanyiwa upasuaji nchini Afrika Kusini.

Lakini kabla ya kwenda Afrika Kusini kwa matibabu, Balama alikuwa akitibiwa nchini kwa mwaka mzima bila mafanikio kabla ya kufikia uamuzi wa kutibiwa nje ya nchi.

Hata hivyo, Helmy alisema changamoto pekee kwa Balama ambayo wanapambana nayo katika kuanza kwake mazoezi na wenzake hofu ya kudhani anaweza kuumia tena na kurudi kukaa nje, lakini akasema itaondoka taratibu.

“Amekaa nje muda mrefu anaona kama anaweza kuumia tena anacheza kwa hofu lakini ni kitu ambacho kitaondoka taratibu kwa kuwa anafanya mazoezi huku tukimfuatilia kwa karibu,” alisema.

Akizungumzia kuanza kwa mazoezi hayo, kocha wa Yanga

Nesreddine Nabi alisema ingawa bado wanafuatilia kurejea kwa Balama lakini kwa jinsi alivyoona mikanda ya kipaji chake anaamini ni mchezaji mzuri anayeweza kusaidia timu.

“Sijawahi kumuona kwa macho nilifika akiwa ameshapata haya matatizo lakini kwa jinsi nilivyoona mikanda yake ni mchezaji sahihi kwa klabu ingawa kwasasa ni mapema kujua ni lini ataweza kuja kucheza kwa kuwa alikaa nj kwa muda mrefu tunatakiwa kumpa muda zaidi awe sawasawa,” alisema Nabi.

SOMA NA HII  MORRISON AUFYATA ..AJISALIMISHA KWA BARBARA....KOCHA WA ASEC AKUBALI MZIKI WA SIMBA...

Kumbukumbu muhimu

Balama alisajiliwa na Yanga akitokea Alliance ya Mwanza na kucheza kwa mafanikio katika kikosi ambacho hata hivyo hakikufanikiwa kutwaa ubingwa kikiwa chini ya kocha Mwinyi Zahera.

Akiwa na Yanga, Mapinduzi anakumbukwa kwa kuisawazishia miamba hiyo bao la kwanza kwa shuti kali la mbali dhidi ya Simba, wakati wa mchezo wa mzunguko wa pili wa kwanza uliomalizika kwa sare ya 2-2.

Katika mchezo huo, Simba ilirudi kipndi cha pili ikiwa inaongoza kwa bao 1-0, kabla ya Deo Kanda kufunga la pili, lakini Balama aliirudisha Yanga mchezoni kwa shuti la mbali lililomshinda kipa Aishi Manula, wakati Mohamed Issa ‘Banka’ kusawazisha la pili.

Balama pia alifunga bao la kichwa cha kuruka akiitanguliza Yanga dhidi ya Biashara katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambalo lilizua gumzo katika ushangiliaji wake, kama aliyekuwa analuliza ‘kuna nini?’.