Home news KABLA HATA YA MPIRA KUAANZA…’FEI TOTO’ AIBUA SHANGWE KWA YANGA ILULU…NABI...

KABLA HATA YA MPIRA KUAANZA…’FEI TOTO’ AIBUA SHANGWE KWA YANGA ILULU…NABI NAYE KAMA KAWA…


Wachezaji Feisal Salum’ ‘ Fei Toto’ na Fiston Mayele wamefunika kwa kupokelewa kwa shangwe wakati Yanga ikiwasili kwenye Uwanja wa Ilulu Lindi.

Yanga imewasili uwanjani hapa Saa 8: 33 mchana kupitia geti la Kaskazini na kisha basi la timu hiyo kuzunguka Uwanjani na  kusimama  karibu na jukwaa kuu.

Wakati wakiwasili mashabiki wa Yanga ambao Leo wameonekana kuwa wengi walilipuka kwa shangwe na mchezaji wa kwanza kushuka kutoka katika basi hilo ni Mukoko Tonombe.

Licha ya wachezaji wengi kushuka na kushangiliwa lakini aliposhuka Mayele shangwe lilizidi na mashabiki wengi kusimama huku wakimpigia makofi lakini shangwe zaidi liliibuka baada ya kushuka kiungo Fei Toto kwani majukwaa matatu ya Uwanja yalilipuka kwa Mayowe huku wengine wakimtaja jina lake.

Feisal aliwaangalia tu mashabiki hao na kutabasamu Kisha kuingia katika vyumba vya kubadilishia nguo.

Pia kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi naye ni mmoja ya watu waliopokelewa kwa shangwe uwanjani hapa pamoja na beki Yannick Bangala.

Feisal ndio kinara wa mabao ndani ya kikosi cha Yanga  msimu huu kwani hadi sasa ameifungia timu hiyo mabao matatu wakati Mayele amefunga mawili sawa na Jesus Moloko.

Yanga itaikabili Namungo majira ya Saa 10:00 jioni katika mchezo unaotarajiwa kuwa mgumu kwani timu hizo hazijawahi kufungana kwenye Ligi Kuu.

SOMA NA HII  FEI TOTO AFUNGUKA YAKE NA YANGA....ADAI IWE ISIWE LAZIMA KIELEWEKE...AGUSIA ALIVYOVUMILIA...