news

NEEMA ZAZIDI KUMIMINIKA KWA WACHEZAJI SIMBA…UONGOZI WATANGAZA ‘SHANGWE’ JIPYA LA KUFA MTU…

admin December 17, 2021 6:15 am


UONGOZI wa Simba SC, umewatengeawachezaji wa timu hiyo bonasi ya Sh 70Mil kwa kila ushindi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports maarufu FA.

Wachezaji hao juzi Jumanne walianza kuvuta mkwanja huo baada ya kuwafunga JKT Tanzania 1-0 katika mchezo wa hatua ya tatu uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar.

Kwa mujibu wa chanzo kutoka ndani ya Benchi la Ufundi la Simba, viongozi wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo, wameongeza bonasi katika michuano hiyo kutoka Sh 50Mil na kufikia 70Mil.

Chanzo hicho kilisema lengo la kuongeza bonasi hiyo ni kuwaongezea morali na hali ya kupambana ili watetee ubingwa huo.

“Wachezaji wa Simba waliocheza na wale waliokaa benchi kila mmoja ana uhakika wa kupata bonasi nzuri ya mchezo uliopita wa FA dhidi ya JKT Tanzania ambao tulishinda bao 1-0.

“Bonasi hiyo ya Sh 70Mil ambayo watapatiwa wachezaji imeongezeka msimu huu, kumbuka msimu uliopita walikuwa wakipata Sh 50Mil.

“Hiyo itawapa hali ya kujituma na kupambana ili tutetee kombe letu, hiyo bonasi inajitegemea tofauti kabisa na ligi na michuano ya kimataifa,” kilisema chanzo hicho.

YANGA CHINI YA MARAJIRI…MAMBO MATAMU YAJA…SIMBA YAANZA NA KIUNGO FUNDI….WAWA ATETEWA.. WAKATI NABI AKIJITETE KWA KUCHEZESHA ‘FULL’ KIKOSI…KOCHA IHEFU ADAI ALITUMIA WACHEZAJI WASIOPATA NAFASI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply