Home news WAKATI YANGA WAKIENDELEA KUTAKATAKA…NABI ALIA NA ‘KAZI CHAFU’ WANAZOFANYIWA…

WAKATI YANGA WAKIENDELEA KUTAKATAKA…NABI ALIA NA ‘KAZI CHAFU’ WANAZOFANYIWA…

 


KOCHA Mkuu wa Yanga, Nassredine Nabi amesema licha ya kuibuka na ushindi 2-1 dhidi ya Tanzania Prisons, kikosi chake kinakutana na wakati mgumu kwani kila timu wanayokutana nayo inacheza kama fainali dhidi yao.

Yanga imefikisha pointi 23 na kuendelea kuwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikifuatiwa na Simba yenye pointi 18 na mchezo mmoja pungufu.

Akizungumzia mchezo wa juzi uliochezwa Uwanja wa Nelson Mandela, Nabi aliwapongeza wachezaji kwa ushindi walioupata kwani walijua ungekuwa mtanange mgumu kutokana na hali iliyokuwa ndani ya timu kutokana na wachezaji 10 walikuwa wagonjwa.

“Kuna wachezaji wetu muhimu walikuwa wagonjwa lakini walisema watacheza na kupambana kwa ajili ya mashabiki ambao wamekuwa wakiwasapoti na wataipigania Yanga na ndivyo walivyofanya, kama kocha napenda kuwapongeza.”

“Kila timu inapocheza na Yanga inacheza kama fainali hivyo tunajiandaa kwani tunajua kila mchezo unakuwa mgumu na wachezaji wanaelewa hilo,” alisema Nabi.

Kaimu Kocha Mkuu wa Prisons, Shaban Kazumba alisema hajafurahishwa na matokeo waliyopata nyumbani kwani walitengeneza nafasi lakini walishindwa kuzitumia na mapungufu ya kikosi chake anakwenda kufanyia kazi.

“Ulikuwa mchezo mzuri, Yanga hawana mpira wa kutisha japo wanaongoza Ligi Kuu, najutia timu yangu kushindwa kutumia nafasi tulizopata,” alisema Kazumba.

Prisons inashika nafasi ya 13 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi nane baada ya kucheza michezo tisa, ikishinda michezo miwili, sare mbili na kufungwa mitano.

SOMA NA HII  KANOUTE ANABAKI AU ANASEPA SIMBA...? UKWELI WOTE UNAOPASWA KUJUA HUU HAPA...