Home news WAKATI ISHU YA CHAMA NA PHIRI IKIWA HEWANI BADO…PABLO AMALIZA KILA KITU...

WAKATI ISHU YA CHAMA NA PHIRI IKIWA HEWANI BADO…PABLO AMALIZA KILA KITU SIMBA..MAGORI ATEMA CHECHE..


KAZI imeanza huko Simba SC. Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia kocha mkuu wa timu hiyo, Pablo Franco kukabidhi rasmi ripoti ya usajili wa majembe mapya katika dirisha dogo lililofunguliwa Desemba 16, mwaka huu na kutarajiwa kufungwa Januari 15, 2022.

Baada ya kukabidhi ripoti hiyo huku akitaja wachezaji anaowahitaji, kesho Jumatatu Bodi ya Wakurugenzi ya Simba itakutana katika kikao kizito kuijadili ripoti hiyo.

Hadi sasa, Simba inahusishwa na usajili wa wachezaji wengi wakiwemo nyota wawili raia wa Zambia Clatous Chama anayecheza RS Berkane na Moses Phiri wa Zanaco.

Akizungumza na Spoti Xtra, kuhusiana na ishu ya usajili, kocha Pablo alisema: “Tayari nimewasilisha mapendekezo ya usajili kwa viongozi, ni kweli kuna maeneo ambayo tunahitaji kuyafanyia maboresho ili kuwa na kikosi bora zaidi.

“Siwezi kuyaweka wazi mapendekezo hayo kwa kuwa ni siri ya klabu, lakini jambo muhimu ni kuwa viongozi wameanza kulifanyia kazi hilo.”

Naye Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Crescentius Magori, alisema: “Kuhusiana na usajili wa nyota wapya kwenye dirisha hili la usajili tulikuwa tunasubiri ripoti ya Kocha Pablo ili kuanza kuifanyia kazi na Bodi inatarajiwa kukaa Jumatatu (leo), kwa ajili ya kufanya tathimini ya ripoti hiyo.”

SOMA NA HII  FENERBAHCE WAMCHEUA TENA SAMATTA....GENK WAMDAKA TENA JUU KWA JUU....