Home Makala BAADA YA KUFIISHA MSIMU MMOJA NA SIMBA…HUYU HAPA NDIYE ONYANGO HALISI NA...

BAADA YA KUFIISHA MSIMU MMOJA NA SIMBA…HUYU HAPA NDIYE ONYANGO HALISI NA MAAJABU YAKE…


TANGU beki wa kimataifa wa Kenya, Joash Onyango alipotua nchini kuitumikia Simba akisajiliwa kupitia dirisha dogo la msimu wa 2020/21 akitokea Gor Mahia ya nchini kwao ametimiza msimu mmoja, huku jina lake likiendelea kuwa juu kutokana na aina ya uchezaji wake.

Onyango alipokewa na utani wa Simba na Yanga kutokana na mwonekano wake, wakampa jina la fastafasta ‘Babu’. Hata hivyo, halikumvunja moyo alikaza uwanjani hatimaye akabadilishwa na kuitwa ‘Chuma’.

Gazeti la Mwanaspoti linakuchambulia aliyofanya Onyango ndani ya msimu mmoja katika mechi za Kariakoo dabi alizocheza.

Mechi ya Desemba 11, 2021 alifanya kazi kubwa ya kupunguza kasi ya straika wa Yanga, Fiston Mayele aliyekuwa anatazamiwa kuwa mwiba kwenye safu yao kutokana na mabao matatu anayomiliki katika ligi.

Ifuatayo ni orodha ya mechi za dabi alizocheza Onyango tangu alipotua Tanzania zilizomsaidia kuondoa kejeli za mashabiki wa Yanga waliopunguza kasi ya kumuita Babu.

JULAI 11, 2020

Onyango alicheza dabi ya kwanza Julai 11, 2020 ikiwa ni muda mfupi aliotoka kusajiliwa dirisha dogo alikopokewa na maneno kuwa kaja kula pensheni ya uzeeni katika soka la Tanzania.

Katika mechi hiyo Onyango alifanya kosa la kumkwatua winga wa Yanga, Tuisila Kisinda dakika ya 30 lililosababisha penalti iliyowapa Yanga bao dakika 31 kupitia kwa Michael Sarpong.

Licha ya Onyango kufanya kosa hilo halikumtoa mchezoni, badala yake alipambana na kuisawazishia timu Simba bao dakika ya 85, akifunga kwa kichwa baada ya kupokea mpira wa kona iliyochongwa na Luis Miquissone.

Baada ya kusawazisha bao aliwajibu waliomuita Babu, kwamba anawaruhusu kuita kila jina wanalotaka na atakachowaonyesha ni kazi uwanjani.

“Sina tatizo kuitwa Babu. Wanaweza wakaita jina lolote wanalotaka, kwani Babu tayari kawafunga,” mwisho wa kunukuu.

JANUARI 14, 2021 -MAPINDUZI

Japokuwa alikosa penalti ya nne huku Meddie Kagere akikosa ya pili, Simba ikipoteza taji kwa mikwaju ya penalti 4-3, Onyango alikuwa kati ya wachezaji walioonyesha kiwango bora.

Penalti hiyo ilikuwa ya kuamua ubingwa wa kombe, lakini Mkenya mwenzake kipa Farouk Shikhalo aliipangua na baadaye alimtania kwa kumwambia “Pole sana kwa kukosa penalti na ubingwa.”

SOMA NA HII  KWA VYOVYOTE VILE....MATANO KUMNG'OA MORRISON SIMBA...CHAMA ATAJWA...

JULAI 3, 2021

Simba ilifungwa bao 1-0 dakika ya 11 kupitia kwa kiungo wa Yanga, Zawadi Mauya. Licha ya matokeo hayo, Onyango alimdhibiti Kisinda aliyemsumbua mara ya kwanza walipokutana Januari 14 na kupitia makosa yake Yanga walipewa penalti.

Onyango alitumia akili kumkaba Kisinda aliyekuwa na mwendo wa kasi – akihakikisha hamruhusu kusogea mara kwa mara ndani ya 18 za Aishi Manula

JULAI 25, 2021- ASFC

Alisaidiana na Pascal Wawa kuimarisha beki ya kati katika fainaliza ASFC iliyopigwa Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma. Timu yake ilitwaa taji kwa ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Thadeo Lwanga.

SEPTEMBA 9, 2021 NGAO YA HISANI

Dabi ya Ngao ya Hisani iliyopigwa Septemba 9 Uwanja wa Mkapa alicheza dakika 26 kabla ya kuumia na nafasi yake ilichukuliwa na Kennedy Juma.

Katika mchezo huo, Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Fiston Mayele dakika ya 11 kabla ya Onyango kuumia.

DESEMBA 11, 2021

Dabi ya Desemba 11, ambayo haikuwa na mbabe alifanya kazi kubwa ya kumdhibiti Mayele kutozoea eneo la kipa wao, Manula.

Umakini wake katika mchezo huo ulimfanya Mayele kupambana na kushindwa kufikia malengo ya kuzifumania nyavu, kwani kuna wakati alikuwa anamuwahi kabla ya kufika eneo lao (kwa kumkabia mbali).