Home news BAADA YA YACOUBA KUWEKWA KANDO…. HIKI HAPA KIFAA CHA TP MAZEMBE KINACHOKUJA...

BAADA YA YACOUBA KUWEKWA KANDO…. HIKI HAPA KIFAA CHA TP MAZEMBE KINACHOKUJA YANGA…

IMEELEZWA kuwa mabosi wa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu,Nasreddine Nabi wapo kwenye hesabu za kumsaka winga wa kazi ili awe ndani ya kikosi hicho kuchukua nafasi ya Yacouba ambaye ni majeruhi.

Yanga inahitaji kufanya maboresho kidogo kwenye eneo la winga ili kuongeza makali kwenye kikosi hicho.

Chico Ushindi winga mwenye miaka 25 anayekipiga ndani ya TP Mazembe anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi wa Yanga ili aweze kuibuka ndani ya kikosi hicho.

Mtendaji Mkuu wa Yanga, Senzo Mbatha hivi karibuni alisema kuwa kwenye upande wa usajili watasubiri ripoti ya Nabi inahitaji nini.

“Ripoti ya kocha itaamua nini kifanyike hivyo mambo yakiwa sawa taarifa zitatolewa,”.

SOMA NA HII  KUELEKEA MICHUANO YA CAF MSIMU UJAO...NABI KAKUNA KICHWA WEEE..KISHA KAFUNGUKA HILI KUHUSU FEI TOTO....