Home news SAA CHACHE KABLA YA DABI…MKWASA ASHINDWA KUJIZUIA..AANIKA TIMU ITAKAYOFUNGWA LEO..AITAJA YANGA..

SAA CHACHE KABLA YA DABI…MKWASA ASHINDWA KUJIZUIA..AANIKA TIMU ITAKAYOFUNGWA LEO..AITAJA YANGA..


MAKOCHA wengine wengine wamedai kuwa Dabi ya leo itategemea na jinsi timu zilivyovyoamka. Lakini Boniface Mkwasa wa Ruvu Shooting yeye amesisitiza kwamba; “Sioni suluhu wala sare, lazima mmoja ashinde kama atatumia nafasi vizuri.” 

Makocha mbalimbali waliocheza na Simba na Yanga wamesema mechi hiyo itakuwa na ushindani wa aina yake. Kocha wa Geita Gold, Fred Felix Minziro alisema; “Hiyo mechi huwa inategemea umeamkaje siku hiyo, kwa sababu kwanza ina presha lakini huwa haitegemei ulikuwa na matokeo gani katika mechi zilizopita. 

Mfano unaweza kusema Simba haijacheza vizuri mechi zao zilizopita hivyo inaweza kupoteza lakini siku ya mechi ya dabi ikaja tofauti mpaka mkashangaa, vivyo hivyo kwa Yanga pia wengine wanaweza kuichukulia poa lakini siku ya mechi hiyo ikaja kivingine kabisa.”

“Ukiangalia timu zote zimefanya usajili mzuri msimu huu hivyo zina ubora kuanzia kwa makipa hadi kwa washambuliaji hivyo yoyote anaweza kushinda inategemea ameamkaje siku hiyo na amekuja na mbinu za maana uwanjani ,” alisema Minziro ambaye ni mchezaji wa zamani wa Yanga.

Naye kocha wa Namungo, Hemedy Morocco alisema; “Sio mechi rahisi kwa sababu ni dabi na timu hizo zinafukuzana kileleni hivyo mechi itakuwa ngumu na inataka utulivu wa akili kwa wachezaji wa timu zote na hata mabenchi yao ya ufundi. Pia mbinu nzuri ndizo zitaamua mechi hiyo.”

Naye kocha wa Ruvu Shooting, Charles Boniface Mkwasa alisema mechi hiyo itakuwa ngumu na yenye ushindani kwani kila timu inata kumpita mwenzake lakini akatabiri kuwa lazima mmoja afungwe hakuna sare siku hiyo.

“Hiyo mechi itakuwa ngumu kwa sababu kila mmoja anataka kumpita mwenzake kulingana na nafasi waliyopo kwenye msimamo sasa hiyo itachangia kuifanya mechi hiyo kuwa nzuri.

“Kutokana na nilivyoziona timu zote kila mmoja ana nafasi ya kushinda endapo atakuwa makini kutumia nafasi na makosa ya mwenzake.Lakini jambo ambalo watu wanatakiwa kujua mechi ya Simba na Yanga huwa tofauti na wengi wanavyofikiria kwani unaweza ukaipa timu fulani nafasi kubwa ya kushinda kulingana na unavyoiona kwa wakati huo lakini ikaja kushinda ile ambayo haipewi nafasi,”alisema Mkwasa ambae ni mwanachama, mchezaji na Kocha wa zamani wa Yanga.

SOMA NA HII  MERIDIANBET WATEKELEZA AGIZO LA DR SAMIA KWA VITENDO...WASHUSHA NEEMA KWA T.Z.K FC..

Geita Gold imeshacheza mechi mbili dhidi ya Simba na Yanga ambapo katika mechi dhidi ya Yanga iliyofanyika kwenye uwanja wa Nyankumbu Geita,Oktoba 2 ilichapwa bao 1-0 na ikafungwa pia na Simba mabao 2-1 katika mchezo uliofanyika Desemba Mosi katika uwanja wa Benjamini Mkapa.

Kwa upande wa Namungo yenyewe ilikubali kipigo cha jioni kwa kufungwa bao dakika ya 90 na Simba na kuufanya mchezo huo uliofanyika uwanja wa Benjamini Mkapa Novemba 3 kumalizikia kwa bao 1-0 lakini ikatoka sare ya bao 1-1 na Yanga katika mchezo uliofanyika Novemba 20 kwenye uwanja wa Ilulu Lindi.

Ruvu Shooting yenyewe ilikubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Yanga katika mchezo uliofanyika Novemba 2 na pia ikapokea kipigo kama hicho kutoka kwa Simba katika mechi iliyochezwa Novemba 19. Simba yenye pointi 17 kwenye msimamo wa ligi inakutana na Yanga ambayo iko kileleni ikiwa na pointi 19. 

Katika kujiandaa na mechi hiyo Yanga ilisalia kwenye kambi yake Kigamboni Jijini Dar es Salaam huku Simba ikihama Mbweni na kuelekea Kisutu kwenye hoteli moja ya kifahari huku mazoezi yakiwa maeneo ya Upanga katika shule moja ya Kimataifa ambayo hairuhusu hata ndege kuchungulia mazoezini.