Home news SIMBA WAFUNGUKA MAENDELEO YA MICHANGO YA UJENZI WA UWANJA..TSH BILIONI 2 ZA...

SIMBA WAFUNGUKA MAENDELEO YA MICHANGO YA UJENZI WA UWANJA..TSH BILIONI 2 ZA TAJWA…

 


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salum Abdallah ‘Try Again” amesema zoezi la wanachama kuchangia fedha za ujenzi wa Uwanja wa klabu hiyo linaendelea vizuri.

‘Try Again’ amesema ndani ya muda mfupi tangu kuzinduliwa kwa zoezi hilo Desemba 17, idadi kubwa ya wanachama wamechangia fedha.

Mpango huu ni wazo la Mwanahisa mkuu Simba, Mohamed ‘Mo’ Dewji ambaye ameahidi kutoa Sh. Bilioni 2 ili wanachama wajazie klabu hiyo ijenge Uwanja wake kuepuka adha inazokutana nao kutumia Uwanja usio wake.

Kwa sasa Simba ina Uwanja wa mazoezi ‘Mo Simba Arena’ uliopo Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na mechi zake za mashindano inatumia Uwanja wa Benjamin Mkapa.

SOMA NA HII  KUHUSU CHAMA KUTUA YANGA...UONGOZI WAAMUA KUANIKA UKWELI HUU...