news

MASHABIKI WA SIMBA WAMUONYESHA CHA MTEMA KUNI MAYELE…APEWA KIBAO CHA KUFA MTU…

admin January 13, 2022 1:27 pm


MASHABIKI wanaodhaniwa kuwa ni wa Simba juzi walijitokeza kwa wingi Bandari ya Dar es Salaam kuwapokea watani zao wa jadi, Yanga ambao waliwasili wakitokea Zanzibar, zaidi walionekana wakimganda straika Fiston Mayele na kupiga naye picha.

Yanga iliondoshwa katika hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi kwa penalti 9-8 mbele ya Azam FC.

Majira ya saa saba, msafara wa Yanga ulishuka bandarini hapo ambapo walikutana na mashabiki wengi waliokuwa wamevalia jezi za Simba huku wakishangilia kwa mtindo anaotumiaga straika wa Yanga, Fiston Mayele inapotokea amefunga bao.

Mashabiki hao walisikika wakiimba: “Tunalitaka kombe letu, tunalitaka kombe letu.” Pia walipata muda wa kupiga picha na Mayele ambaye ni kinara wa utupiaji ndani ya Yanga kwenye ligi akiwa na mabao matano na pasi moja.

Hassan Bumbuli, Mkuu wa Kitengo cha Habari Yanga, alisema kuwa hesabu zao kwa sasa ni kwenye ligi.

“Bado tuna kazi ya kufanya hasa baada ya kushindwa kutwaa taji la Mapinduzi na malengo yetu ilikuwa ni kutetea ubingwa wetu, kilichotokea ni matokeo,” alisema Bumbuli.

BAADA YA KUANZA KWA KASI YANGA…NKANE AKUTWA NA GONJWA LA AJABU..KUKAA NNJE MPAKA…. RASMI…ISHU YA MNIGERIA NA SIMBA IMEISHA..KAMA KAWA BARBARA ASISITIZA SAPRAIZI INAKUJA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply