PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba, amesema wana ratiba ngumu jambo linalowafanya kutumia nguvu kubwa kusaka ushindi.
Juzi Jumamosi, Simba ilicheza mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar uliochezwa Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro na mcheo kuisha kwa timu zote kugawana alama moja.
Kabla ya mchezo huo, Simba ilitoka kupoteza mbele ya Mbeya City kwa kufungwa bao 1-0.
Jumatano ijayo watakuwa mkoani Kagera kupambana na Kagera Sugar. Hizi ni mechi za ligi kuu. Kisha Januari 30, watawakaribisha Dar City kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, ukiwa mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam hatua ya 32 bora.
Pablo amesema: โTumetoka Mbeya kucheza, kisha Mtibwa Sugar, baada ya hapo bado tuna kazi nyingine, ratiba bado inaonesha kwamba wachezaji wanapaswa kucheza muda wote.
โKatika hilo wapo wachezaji ambao ilinipasa kuwapumzisha ikiwa ni pamoja na Rally Bwalya ambaye alikuwa amechoka, hivyo tuna kazi kubwa yakufanya katika mechi zetu zijazo.โ