Home news KISA UJIO WA CHAMA…PABLO AFUMUA KIKOSI CHOTE SIMBA..KAGERE NA MUGALU MMOJA KUMPISHA...

KISA UJIO WA CHAMA…PABLO AFUMUA KIKOSI CHOTE SIMBA..KAGERE NA MUGALU MMOJA KUMPISHA ….


BAADA ya ujio wa Clatous Chota Chama ndani ya Simba ni wazi sasa Kocha Pablo Franco itamlazimu kubadili mfumo ambao utawafanya nyota wa timu hiyo, Clatous Chama, Larry Bwalya na Pape Ousmane Sakho kuweza kucheza kwa pamoja ndani ya kikosi hicho.

Kabla ya ujio wa Chama, kocha Pablo Franco alikuwa akipendelea kutumia mfumo wa 4-2-3-1 jambo ambalo lilikuwa linawafanya Bwalya na Sakho kucheza kwa pamoja katika eneo la viungo washambuliaji.

Katika mfumo huo wachezaji wawili walikuwa wanacheza kama viungo wa ulinzi huku katika wale watatu wa juu Bwalya alikuwa akicheza katikati huku wawili wa pembeni alikuwa akicheza Sakho na Morrison au Sakho na Kibu Denis.

Lakini baada ya ujio wa Chama lazima mambo yatabadilika kimfumo endapo Kocha Pablo Franco atahitaji kuwatumia wachezaji hao wote katika mchezo mmoja ambapo itamlazimu kubadilisha mfumo kutoka 4-2-1 kwenda kwenye 4-3-3.

Ambapo katika mfumo huu viungo watatu watakuwa Bwalya na Chama ambao itabidi washuke chini kucheza pembeni ya kiungo mmoja mkabaji kati ya Jonas Mkude au Thadeo Lwanga kisha wenyewe wakiwa juu yao.

Kwa upande wa washambuliaji watatu wa juu, Bernard Morrison na Pape Ousmane Sakho watacheza katika winga ya kulia na kushoto huku mshambuliaji wa kati akitarajiwa kuwa kati ya Meddie Kagere au Chris Mugalu.

SOMA NA HII  ISHU YA DEREVA WA SIMBA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUENDESHA GARI KINYUME NYUME ...UKWELI UKO HIVI...