Home news KURUDI KWA CHAMA….HAYA HAPA MAMBO MATANO MAKUBWA ALIYORUDI NAYO BONGO…

KURUDI KWA CHAMA….HAYA HAPA MAMBO MATANO MAKUBWA ALIYORUDI NAYO BONGO…


AMERUDI. Ndiyo kauli unayoweza kuitumia kwa sasa baada ya Simba kumrejesha kiungo wake, Clatous Chota Chama ‘Triple C’ aliyekuwa anakipiga RS Berkane ya Morocco.

Hii ni mara ya pili kwa nyota huyo kujiunga na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba baada ya mwaka 2018 kujiunga rasmi kwa mara ya kwanza akitokea klabu ya Lusaka Dynamos ya nchini kwao Zambia.

Kurejea kwake kumeamsha shangwe kwa mashabiki na wapenzi wa klabu hiyo ambayo imekuwa ikitawala msimu wa 2020/2021, ikionekana kuwa na mafanikio kwa timu za Bongo kwa kubeba Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) na kufika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yafuatayo ni mambo matano ambayo Chama atayaongeza, sio tu kwa Simba bali hata kwenye Ligi Kuu Bara kwa ujumla.

KUONGEZA USHINDANI

Jambo la kwanza analotakiwa kufanya mchezaji anaposajiliwa ni kuweza kuisaidia timu kufikia malengo waliyojiwekea kabla ya msimu kuanza.

Hakuna shaka juu ya uwezo wake kuanzia kufunga na kutengeneza nafasi za mabao kwa wengine, jambo ambalo alishaonyesha msimu uliopita akihusika katika mabao 23 ya timu yake, huku akifunga manane na asisti 15.

Ligi ndio kwanza iko katika mzunguko wa 12, huku mbio za ubingwa zikionekana zinaelemea upande wa Simba na Yanga kutokana na timu hizo kupishana pointi chache, jambo ambalo litazidi kuweka presha kileleni.

KUZIBA PENGO

Wakati Chama anaondoka Simba nafasi yake ilikuwa inaonekana wazi huku baadhi ya wachezaji waliosajiliwa kama mbadala wake wakionekana kuvaa viatu vikubwa vilivyowashinda.

Winga Pape Ousmane Sakho anaonekana kuwa kwenye kiwango bora na urejeo wake utaendelea kuleta matunda kwa klabu hiyo katika safari ya kuletea Kombe la Ligi Kuu Bara na la Shirikisho la Azam (ASFC).

KUONGEZA MVUTO

Msimu uliomalizika Ligi Kuu Bara ilikuwa na mvuto wa aina yake, jambo lililowashawishi mashabiki wengi kwenda kuangalia mpira uwanjani na wengine kutazama kupitia runinga.

Hayo yote kwa pamoja yalikuwa yanaletwa na soka safi lililokuwa likipigwa na ‘Mwamba wa Lusaka’ ndani ya uwanja kupitia pasi kali za ‘upendo’ alizokuwa anazicheza.

SOMA NA HII  ARSENAL SHANGWE YAREJEA KITAA, GABRIEL AFANYA KAZI CHAFU

LIGI KUFUATILIWA ZAIDI

Katika misimu minne iliyopita Ligi Kuu Bara imepiga hatua kubwa na ikipata nafasi nne za uwakilishi wa timu kwenye michuano mikubwa ya soka barani Afrika kwa ngazi ya klabu.

Mafaniko hayo hayakuja kwa bahati mbaya bali yametokana na ushindani, ubora wa timu na wachezaji ambao ndio wahusika wakuu uwanjani.

Kurudi kwake tena kutaifanya ligi kuendelea kuangaliwa zaidi kutokana na kiwango alichokionyesha kwa msimu uliopita.

KUBURUDISHA

Ubora wa wachezaji pamoja na vituko mbalimbali vya ndani na nje ya uwanja ndio burudani kubwa ambazo mashabiki wengi wa soka hupenda kuona.

Burudani hizo zilikuwa zinaongozwa na Chama ambaye kiwango chake kilikuwa burudani tosha kwa mashabiki sio wa Simba tu ambao humshabikia la hashaa, bali hata wale wapinzani wao wakubwa Yanga walifanya soka litazamwe na kushangiliwa viwanjani.

Msimu huu kivutio kikubwa kimekuwa kwa mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele ambaye tangu ajiunge na timu hiyo licha ya umahiri wake wa kufumania nyavu ila amekuwa kipenzi cha mashabiki wengi kutokana na aina yake ya ushangiliaji.