Home news MORRISON, MANULA NA ONYANGO OUT SIMBA….LWANGA NDANI SAFARI YA SIMBA ZANZIBAR…

MORRISON, MANULA NA ONYANGO OUT SIMBA….LWANGA NDANI SAFARI YA SIMBA ZANZIBAR…

[the_ad id="25893"]

 


WASHINDI wa pili kwenye kombe la Mapinduzi Zanzibar Simba wameondoka Dar es Salaam saa 3:30 asubuhi ya leo, kuelekea mashindano hayo yaliyoanza jana (Jumapili), katika Uwanja wa Amaan.

Katika msafara huo wa Simba uliofika Bandarini Posta saa 3:00 asubuhi hawakuonekana wachezaji watatu ila wengine wote walikuwepo kwa ajili ya kwenda kuipigni timu katika mashindano hayo.

Wachezaji ambao hawakuonekana katika msafara huo wapo, Benard Morrison, Aishi Manula na Joash Onyango ila wengine wote walikuwa sehemu ya kikosi na watafika Zanzibar mchana kishakupokelewa na Mratibu, Abbas Ally aliyetangulia siku mbili nyuma.

Katika hatua nyingine kwenye msafara huo alikuwepo kiungo wa Kiganda Taddeo Lwanga aliyekuwa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu kutokana na majeraha ya mguu yalikuwa yakimsumbua mpaka kurudi kwao kwa matibabu zaidi.

Kocha wa Simba, Pablo Franco amesema kikosi cha Simba kinakwenda katika mashindano hayo kikiwa na mlengo wa kuchukua taji hilo la kwanza msimu huu kwani ni miongoni mwa mafanikio wanayotamani kuyapata chini yake.

Pablo amesema Lwanga ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa katika msafara huo kutokana maendeleo yake ni mazuri na anategemea kumtumia katika mashindano hayo ili kuona namna gani atarudi katika hali ya ushindani.

“Maandalizi yetu katika mashindano haya ni mazuri ndio maana tunakwenda na kikosi kizima ili kupata uwanja mpana wa kutumia wachezaji wote kwa nyakati tofauti kulingana na mechi zitakavyokuwa,” amesema Pablo.

SOMA NA HII  RASMI...SERIKALI YAINGILIA KATI KIPIGO CHA MWAKINYO...WAZIRI ATOA MSIMAMO HUU...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here