Home news PAMOJA NA KUSOTA BENCHI …MAKAMBO AVUNJA UKIMYA YANGA…AFUNGUKA KUHUSU YANAYOMKUMBA…

PAMOJA NA KUSOTA BENCHI …MAKAMBO AVUNJA UKIMYA YANGA…AFUNGUKA KUHUSU YANAYOMKUMBA…


HERITIER Makambo, mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa ipo siku atafunga kwenye ligi kwa kuwa ni suala la muda hana mashaka nalo.

Kwenye ligi Yanga ikiwa imefunga mabao 22 katika mechi 12 ambazo imecheza, nyota huyo raia wa DR Congo hajafanikiwa kufunga wala kutoa pasi ya bao.

Akizungumza na gazeti la  Championi  Makambo alisema kuwa anatambua kwamba mashabiki wanapenda kuona akifunga ila muda bado haujafika.

“Mashabiki wanapenda kuona nafunga hata mimi pia ninapenda kufanya hivyo lakini ni suala la kusubiri kwani bado kuna mechi za kucheza na mechi zipo nyingi hivyo ipo siku nitafunga,” alisema.

Nyota huyo amecheza mechi 10 kati ya 12 na kuyeyusha dakika 279 kwenye mechi za ligi.

SOMA NA HII  KISA TABIA ZAKE ZA 'KIHUNI' NDANI NA NNJE YA UWANJA...SIMBA YATAKIWA KUMPA ADHABU HII MORRISON...