Home Uncategorized HUYU HAPA NI MBABE WA SARE, YANGA NA SIMBA WANAJUA SHUGHULI YAKE

HUYU HAPA NI MBABE WA SARE, YANGA NA SIMBA WANAJUA SHUGHULI YAKE


TANZANIA Prisons, iliyo chini ya Kocha Mkuu Adolf Rishard ndani ya Ligi Kuu Bara ni mabingwa wa kulazimisha sare kwenye mechi zao.

Wamecheza jumla ya mechi 30 wakiwa wanaongoza kwa kucheza mechi nyingi zaidi na pointi zao 41 kibindoni jumla ya mechi 14 walililazimisha sare.

Shughuli yao Simba ile iliyokuwa chini ya Kocha Mkuu, Patrick Aussem ilihaha Uwanja wa Uhuru na kukubali kugawana pointi moja moja.

Imeshinda mechi tisa ndani ya ligi ambazo ni sawa na dakika 810 huku ikichapwa mechi 7 sawa na dakika 630.

Yanga inashikilia rekodi ya kuwatungua mwanzoni kabisa Uwanja wa Samora kwa bao 1-0 lilifungwa na Patrick Sibomana kwa pasi ya Upendo ya Abdulaziz Makame.


Mchezo wa mzunguko wa pili uliochezwa Uwanja wa Taifa Yanga liambulia kugawana pointi moja na Prisons baada ya dakika tisini kukamilika kwa sare tasa.

SOMA NA HII  MANARA AFUNGUKA KUHUSU MO DEWJI NA AINA YA WATU ANAOWAPENDA