Home Habari za michezo KUELEKEA UCHAGUZI MKUU YANGA….WANNE WAKATWA MAPEMAAAA….MABOSI WAPYA HUENDA WAKAWA KATI YA HAWA...

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU YANGA….WANNE WAKATWA MAPEMAAAA….MABOSI WAPYA HUENDA WAKAWA KATI YA HAWA 22…


Jumla ya wagombea 22 wamepitishwa kuendelea na mchakato wa uchaguzi katika nafasi za wanaosaka nafasi za ujumbe huku wengine 4 wakikatwa.

Taarifa ambayo imetolewa na kamati ya uchaguzi ya Yanga imeonyesha wagombea wa nafasi ya ujumbe waliopitishwa ni Said Kambi,Salum Mkemi,Gerrard Kihinga,Saad Khimji,Semi Yusuf,Seif Gulamali,Munir Seleman.

Wengine ambao wamepitishwa ni Issa Mangungu,Wilbard Kilenzi,Salim Rupia,Sylvester Haule,Sindilo Lyimo,Leevan  Muro,Omary Kimosa.

Pia wamo Edgar Chibura, Philip Haule, Alexander Ngai, Dominic Albinius, Benjamin Mwakasonda, Rodgers Gumbo, Yanga Makaga,Samwel Lukumay na Hussein Nyika.

Wagombea ambao hawakupitishwa kugombea ujumbe kwa dosari mbalimbali ni ni Mustapha Himba, Kara Remtullah, Thobias Lingalangala na Sindilo Lyimo.

Kwa mujibu wa hutaji la katiba ya Yanga wagombea hao 22 wanakwenda kuwania nafasi tano za ujumbe kwa upande wa uwakilishi.

SOMA NA HII  KISA SIMBA....NAMUNGO WATUA DAR KIBABE....'PAPA'AH MOLINGA AONGOZA MSAFARA...PLANI ZAO NIKO HIVI...